AZAM jeuri bwana! Wamekodi ndege kutoka Unguja kwenda Pemba
kucheza robo fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Cloves na
ikawasubiri wakerejea nayo Unguja.
Tukio hilo walilifanya jana Jumatano baada ya waandaaji wa michuano hiyo kudai kwamba hawana fedha za kuileta Cloves Unguja.
Azam awali iligoma kwenda Pemba kwa vile Cloves
ilitakiwa kuifuata Azam kabla ya waandaaji kulia kwamba hawana fedha za
kuileta timu hiyo Unguja na kuirudisha.
Msemaji wa mashindano hayo, Farouk Karim, alisema:
“Sisi hatuna uwezo wa kuileta Cloves tumezungumza na uongozi wa Azam
wamekubali kubeba gharama zote wao wenyewe, wataipeleka timu yao na
kurudi.”
Kwa upande wa Meneja wa Azam, Jemedari Said,
alisema: “Tumekodi chata (ndege ndogo) mbili za Zan Air zina uwezo wa
kubeba watu 13 kila mmoja, tumefika salama hapa Pemba na zitatusubiri,
baada ya mechi tu tunageuza, mechi ya Simba na Chuoni tutakuwa uwanjani
usiku hapo Unguja.”
Azam ilicheza na Cloves jana Jumatano saa nane mchana.
Michuano ya kuwania Kombe la Mapinduzi ni maalum kwa ajili ya kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar
No comments:
Post a Comment