Johari. |
Wakizungumza na Ijumaa baadhi ya watu waliobahatika kuiona picha hiyo wamesema kuwa kitendo cha Johari kuweka picha hiyo ni sawa na kuwarusha roho wawili hao kwamba yeye atakuwa wa kwanza kuolewa kabla ya Chuchu na Ray kufunga ndoa.
Ray na Chuchu.
“Unajua kila mtu ana njia yake ya kufikisha ujumbe, kitendo cha hivi
juzi Ray na Chuchu kujiachia bila ya kificho katika Viwanja vya Leaders
Club, ambapo kulikuwa na uchaguzi wa viongozi wa Bongo Movie ni sawa na
kumwambia Johari hana chake ndiyo maana na yeye ameamua kurudisha
kijembe kwa staili ya kuweka picha aliyovaa pete ya ndoa ili kuonyesha
kuwa yeye ataolewa ila Chuchu atachezewa tu na kutupwa,” alidai mmoja
wao.
Baada ya kusikia taarifa hizo kutoka kwa wadaku hao Ijumaa lilimuendea hewani Johari ambapo alipokea simu na kusema atafutwe muda mwingine kwani alikuwa yupo bize.
No comments:
Post a Comment