14 January 2014

HAKIKA HUYU NDO MSANII WA HIP-HOP ALIYEFUNIKA KATIKA SHOW KWA MWAKA 2013

Anajulikana kwa jina la JOH MAKINI msanii wa Hip Hop anayewakilisha mko wa ARUSHA Tanzania, kwa mwaka huu 2013 nilibahatika kuwazunguka nae kuwa kama dj wake katika show zake alizokuwa akipiga karibia Tanzania nzima. Nadiriki kusema kwa
mwaka huu Joh Makini ndio msanii wa Hip Hop aliyepiga show nyingi kuliko msanii mwingine na kama yupo basi naomba niambiwe ili niweke kumbukumbu vizuri. Kwa mimi tu kama DJ CHOKA show nilizofanya naye dj ni show 24 kwa mwaka huu na show ya mwisho ilikuwa Xmas pale Dar Live sasa kuna show nyingine alizoenda kama yeye mwenyewe ukijumlisha na matamasha mengine makubwa so inaweza kufika show 50 nakuendelea. Nanukuu ujumbe wake huu aliouandika kwenye account yake ya Facebook
“Muziki wangu na kila nilichokifanya kimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na Mapenzi ya Mwenyezi Mungu na sapoti yenu teamweusi watu wa muziki mzuri asanteni sana bila nyinyi hakuna mimi nawatakia heri ya mwaka mpya wenye amani na mafanikio

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname