20 January 2014

BINTI AFUNGUKA JUU YA FREEMASON BAADA YA KUWA MFUASI NA SASA AMEOMBEWA NA KUWA HURU..


Binti huyu alisema kuwa alijiunga freemason akiwa na miaka kumi na tano, na ndani ya miaka yote hiyo alishiriki kikamilifu katika mikutano ya rohoni ya chama hicho. Alieleza hayo baada ya maombezi kutoka kwa Mch. Frank Andrew wa kanisa la Ufufuo na Uzima.

Wakitoa ushuhuda, wazazi wa binti huyo walisema kuwa, walianza kuona mabadiliko baada ya kuona binti huyo hali chakula wala maji kwa mida mrefu bila kukonda. Ndipo walipoamua kumleta kanisani Ufufuo na Uzima Arusha, wakiwa na lengo kuwa aje afunguliwe kutokula kwake.

Baada ya maombezi binti huyo akafunguliwa roho za freemason, na baada ya kuwekwa huru ndipo alipojidhihirisha na kueleza aliyokuwa akifanya.

Pichani Binti huyo anaonyesha alama ambazo walikuwa wakizitumia ili kutambuana....

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname