Sio kwamba mastaa wa zamani wa bongofleva hawakuwa wanapata chochote
kwenye malipo kutokana na kazi zao bali imefahamika kwamba mipangilio
na matumizi mazuri ya fedha havikuzingatiwa sana kwa baadhi ya Wasanii
wachache ambao walibahatika kuzipata
pesa nyingi zilizotokana na mauzo ya kanda na show.
pesa nyingi zilizotokana na mauzo ya kanda na show.
Wasanii wengi wa bongoflevani sasa hivi wameshtukia mchezo ndio maana
wengi wao wanaingia kwenye headlines za kuonyesha mali zao kama nyumba
na magari siku kadhaa tu baada ya kusikika kwenye chati za bongofleva
ambapo hii kwa kiasi kikubwa ni kutokana na malipo ya show zao, wengine
mauzo ya nyimbo kwenye miito ya simu, dili za makampuni na ishu
nyingine.
Barnaba ni miongoni tu mwa waimbaji wenye talent zao na amekua akifanya
showz mbalimbali hata nje ya Tanzania pamoja na kupata dili za
mashirika/taasisi mbalimbali na kufanya nao kazi zikiwemo za ubalozi
mfano Pepsi, Barclays Bank na wengine kama unavyoweza kuona moja ya
stori zake za mwaka 2013.
Baada ya kuiweka hiyo picha ya nyumba kwenye instagram yake Barnaba aliiambatanisha na hiki hapa chini
Barnaba
ameidondosha hii picha ya nyumba yake mwezi mmoja tu baada ya
kudondosha picha za gari lake jipya ambalo ni Toyota Mark X.
No comments:
Post a Comment