31 January 2014

ANGALIA PICHA YA KIJANA ALIYEFARIKI WAKATI AKITAKA KUWEKA REKODI YA DUNIA YA GUINNESS


Roy akijaribu kujinasua kwa mikono baada ya kuwa amenasa nywele zake.
Mchezaji michezo ya hatari amefariki dunia katika harakati zake za kuweka rekodi ya dunia wakati akijaribu kuvuka juu ya mto mmoja kwa kutumia waya mwembamba ulioungwa katika nywele zake.

Sailendra Nath Roy, miaka 50, alikuwa nusu ya safari yake kupitia mkogo huo ndipo mtindo wake wa nywele uliponasa kwenye kifundo cha waya aliokuwa akisererekea na kubaki akining'inia angani kwa takribani dakika 25.

Licha ya majaribio kadhaa kujinasua mwenyewe, inaaminika Roy kisha alipatwa na mshituko wa moyo na kufariki dunia.

Roy, mlinzi katika Jeshi la Polisi wa West Bengal, tayari alikuwa akishikilia rekodi ya dunia ya Guinness kwa kusafiri umbali mrefu zaidi kwenye waya mwembamba kwa kutumia nywele zake.


Takribani watu 1,000 walijitokeza kwenda kumshuhudia akijaribu na kuvunja rekodi hiyo juu ya Mto Teesta mjini Darjeeling, ambao ni karibu futi 10,000 juu ya usawa wa bahari, ndipo ajali hiyo isiyo ya kawaida ilipotokea.
Roy alijaribu kujinasua mwenyewe baada ya mtindo wake wa nywele kunaswa kwenye kifundo katika waya na kisha kujaribu kuendelea kuvuka akitumia mikono yake pekee.
Hatahivyo, vyombo vya habari mjini humo vilisema kisha baadaye akapatwa na mshituko wa moyo.
Waokoaji walimshusha chini kutoka Daraja hilo la Kutawazwa takribani dakika 45 baadaye.
Alipelekwa katika hospitali ya karibu lakini alithibitishwa kufariki wakati alipofikishwa hospitalini hapo.
Mashuhuda walisema washangiliaji mwanzoni walishindwa kubaini Roy alikuwa kwenye matatizo sababu ya kelele zilizokuwa zikitoka kwa umati huo.
Mchezaji huyo wa michezo ya hatari amewahi kushikilia rekodi kadhaa za Guinness duniani kwa kuvuta magari kwa kutumia nywele zake.
Alivutia wengi duniani mwaka jana pale alipokokota garimoshi lenye tani 42 kwa umbali wa mita 2.5.
Mwaka 2011, alisafiri umbali wa futi 270 juu ya waya mwembamba, ambao ulishikizwa kwenye nywele zake.
Kamishna wa Polisi wa Siliguri, K. Jairaman alisema Roy hakutakiwa kupata ruhusa muhimu kwa ajili ya mchezo huo wa hatari, akiongeza kwamba Roy hakuwa kazini wakati alipofikwa na mauti.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname