Hivi
karibuni nilifanya mazungumzo na watangazaji wakongwe watatu nchini,
Godwin Gondwe aka Double G ambaye kwa sasa ni lecturer wa chuo kikuu cha
Tumaini na pia msomaji wa habari wa ITV na shughuli zingine, Sosthenes
Ambakisye aka SOS B ambaye kwa sasa hayupo tena kwenye utangazaji na
Basil Mbakile ambaye kwa sasa ni mtangazaji/reporter wa idhaa ya
Kiswahili ya BBC.
Wote
hawa kwangu ni miongoni mwa watu walionivutia kwenye kazi ya utangazaji
(role models) na niliwatafuta kwa lengo la kutaka kushare nao hofu
nilionayo sasa kwenye vipindi vya burudani katika redio nyingi za
Tanzania. Hofu hiyo ni kuwa kwa mwaka 2013, vipindi vya radio vya
burudani vimeshuka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka iliyopita.
Kushuka
kwake kunatokana na watangazaji wengi kufanya kazi kwa mazoea,
kutojiandaa, kukosa vitu exclusive vya kuweka kwenye vipindi vyao,
udhaifu katika kufanya interview na wasanii, uchaguzi wa nyimbo
unaogubikwa na upendeleo hasa kwa wasanii wa nyumbani na mambo mengine.
Wote kwa pamoja walikiri kuwepo kwa tatizo hilo.
Katika
maongezi hayo ambayo mwakani naweza kuja kuyaandikia makala maalum
kuhusiana na hilo, Godwin Gondwe aliniambia kuwa watangazaji wengi
wanatanguliza umaarufu badala ya bidii ya kazi. Alisema watangazaji
wengi hasa wa redio kubwa wamelewa umaarufu walionao ambao unawafanya
wasijitume tena kama walivyokuwa wakifanya zamani.
SOS
B alinieleza kuwa watangazaji wa sasa hawajiandai kabisa na hivyo
vipindi vyao kushindwa kuwa na vitu muhimu vya kuwalisha wasikilizaji.
Alimaanisha kuwa, vipindi vingi hukamilika na kumwacha msikilizaji bila
kitu kinachoweza kumuongezea maarifa au elimu mpya kuhusu burudani na
wasanii licha ya kuburudika.
Basil
Mbakile alinieleza kuwa watangazaji wengi wanashindwa kuwa wabunifu
kwakuwa wanakosa mapenzi ama ‘passion’ ya utangazaji na hivyo
kuuchukulia utangazaji kama ajira kumpatia tu ujira.
Pamoja
na hofu hiyo wapo watangazaji wa radio wanaoendelea kujituma kuvifanya
vpindi vyao viwe bora zaidi. Kwa mwaka 2013, hawa ni watangazaji bora
zaidi upande wangu na ambao naamini wataongeza bidii zaidi mwaka 2014
ili wawe bora kupita walivyokuwa mwaka 2013.
1. Millard Ayo – Amplifaya na Clouds FM Top 20
Kwangu
na kwa wengine wengi, Millard Ayo ndio mtangazaji bora zaidi Tanzania
kwa sasa. Kwa miaka miwili mfululizo, 2012 na 2013, Millard amekuwa
akiongoza kura za maoni za Bongo5 kuhusu mtangazaji anayesikilizwa zaidi
Tanzania.
Godwin
Gondwe anamchukulia Millard kama mtangazaji anayejituma zaidi kuliko
wote Tanzania na kwamba kama angekuwa anafanya kipindi muda sawa na
yeye, basi angekuwa anampa hofu sana. Naye mtangazaji mkongwe, Masoud
Masoud wa TBC Taifa, aliwahi kusema kwenye kipindi cha Mkasi mwaka huu
kuwa, Millard ndiye mtangazaji anayemkubali kwa sasa na humkumbusha enzi
zake za ujana wake.
Japo
si kituo chake cha kwanza kuanza kazi, jina la Millard lilianza
kufahamika nchini kupitia kipindi cha Milazo 101 cha Radio One. Sauti
yake yenye mamlaka na ubunifu hewani, ulikifanya kipindi hicho kuwa
maarufu kuliko vingine vya burudani katika radio hiyo inayomilikiwa na
kampuni ya IPP.
Kuondoka
kwake Radio One kulikuwa ni pigo kubwa lakini lenye neema kwa Clouds
FM. Alihamia Clouds FM na kuanzisha kipindi kipya kiitwacho Amplifanya
ambacho kilichukua nafasi ya kipindi cha nyimbo za kiafrika, Bambataa.
Haikuchukua muda kipindi cha Amplifanya kikawa miongoni mwa vipindi bora
kabisa Clouds FM. Kipindi hicho pia ni miongoni mwa vipindi
vinavyoiingizia fedha nyingi redio hiyo na kumfanya Millard kuwa
miongoni mwa watangazaji wa kituo hicho wanaolipwa mshahara mkubwa
zaidi.
Leo
hii Millard ni miongoni mwa watangazaji bora Tanzania na wanaosikilizwa
zaidi. Si maarufu tu redioni bali pia ndiye mtangazaji wa Tanzania
mwenye mashabiki wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Ana zaidi ya
followers 75,000 kwenye Twitter huku Facebook akiwa na likes zaidi ya
153,000.
Umaarufu
wake kwenye mitandao ya kijamii umemfanya ageuke brand na kuyavutia
makampuni makubwa kama CRDB Bank, Fast Jet na mengine kudhamini kile
anachotweet. Tweets zake tu zinamuingizia fedha huku akimiliki pia
website yake binafsi yenye wasomaji lukuki na yenye matangazo mengi.
Kwa
mshahara anaoupata, kazi ya uripota wa DSTV, ubalozi wa Fastjet,
website yake, deal za voice-overs na mambo mengine, Millard anaingiza
takriban ama zaidi ya shilingi milioni 10 kila mwezi.
Millard
ni zaidi ya mtangazaji, bali ni mwandishi mwenye ‘pua ya habari’ (nose
for news) huku akiongoza kwa kuja na angle za kipekee za habari zenye
mvuto kwa watu (human interest stories) zinazokifanya kipindi chake cha
Amplifaya kuteka matangazo ya jioni siku za wiki.
Pamoja
na kupata mafanikio hayo, Millard ameendelea kuwa mchapakazi, simple,
mtu anayejituma kutafuta habari hata sehemu za mbali kabisa, mcheshi na
mtu wa watu. Hakuna shaka kuwa, Millard ana mustakabali wa nguvu kwenye
fani hiyo. Ni mfano wa kuigwa kwa watangazaji wengine na hazina kubwa
kwa wazazi wake, Clouds Media Group na hata taifa kwa ujumla.
2. Hamis Mandi aka B12 – XXL Clouds FM
Kwa
muda mrefu, XXL kimeendelea kuwa kipindi namba 1 cha burudani nchini.
Kama wimbo wa msanii usipochezwa kwenye XXL, basi wimbo huo una kasoro.
Yeye mwenyewe B-Dozen anajiita mfalme wa vipindi vya mchana na hakuna
msanii yeyote mkubwa wa Bongo ambaye hajawahi kuhojiwa na mtangazaji
huyu mahiri. Kwangu mimi, B-Dozen ndio roho ya XXL ambaye kama
asipokuwepo, hakuna mtangazaji anayeweza kukipa kipindi hicho ladha
iliyozoeleka. Ndicho kipindi ambacho nyimbo kali za wasanii
zimezinduliwa exclusively mwaka 2013. Mwaka huu B12 alitajwa kwenye
orodha ya Top Ten Most ya Channel O ya watangazaji bora wa Afrika huku yeye akikamata nafasi ya 9.
3. Raheem Da Prince – The Switch, Times FM
Utangazaji
wa Raheem na uelewa wake wa muziki, hunifanya nivutike sana kusikiliza
kipindi chake cha The Switch kila Jumamosi. Japokuwa Madj wa show hiyo
DJ D-Ommy na DJ KU ni sehemu ya kivutio cha show hiyo, ufuatiliaji wa
Raheem kuhusiana na muziki wa Marekani na kwingine, hunifanya nitoke na
elimu kubwa kila nisikilizapo show yake.
Amekuwa
akijituma sana kuchambua matukio ya muziki yakiwemo kuchambua album za
wasanii wa Marekani na mambo mengine. Mwaka huu nilifurahia zaidi
uchambuzi alioufanya kwa kushirikiana na Reuben Ndege aka Nchakalih,
Hermy B na Miss East Africa 2012, Jocelyne Maro wa album ya Jay Z, Magna
Carta Holy Grail. Sijawahi kusikia uchambuzi mkali wa muziki kama huo
kwenye redio yoyoye ya Tanzania kwa miaka mingi.
4. Vanessa Mdee – The Hitlist, Choice FM
Vanessa
Mdee hutangaza kipindi cha The Hitlist cha Choice FM na ndio sehemu
yangu iliyosalia ya kusikiliza nyimbo mpya za Marekani ambazo kwa sasa
ni nadra kuzikisia kwingine. Awali show niliyokuwa nikiitegemea kwa
kusikiliza selection nzuri ya nyimbo mpya za Marekani ilikuwa ni kwenye
The Cruise ya Choice FM kipindi ambacho Steve Kabuye alikuwa anatangaza
bado. Napenda uchangamfu wa Vee Money kwenye show yake na uelewa mzuri
wa ngoma za nje.
5. Jabir Saleh – The Jump Off, Times FM
Namchukulia
Jabir Saleh aka Kuvikacha kama maktaba ya muziki wa vijana. Nadiriki
kusema ni watangazaji wachache sana Tanzania wenye uelewa wa muziki wa
Hip Hop kama alionao Jabir. Ukisikiliza kipindi cha The Jump Off, hakuna
shaka kuwa elimu yako kuhusu Hip Hop itapanuka zaidi na kamwe huwezi
kujuta kumsikiliza.
6. Sam Misago – Power Jams , EA Radio
Power
Jams na XXL ndivyo vipindi vyenye ushindani zaidi kwa siku nyingi
katika vipindi vya mchana. Akiwa amejipa jina ‘The Presenter’s
President, Sam ni miongoni mwa watangazaji wenye mashabiki wengi mchana.
7. Bizzo – Show Time; New Chapter , RFA
Umaarufu wa Bizzo ulianzia Ebony FM, Iringa ambako alikuwa akifanya show iitwayo The Splash. Kwa sasa Bizzo ambaye jina lake halisi ni Renatus Kiluvya, ni mtangazaji wa kipindi cha Show Time cha Radio Free Africa. Kwa kiasi kikubwa amejitahidi kuliziba pengo la Kidbwoy aliyekuwa amezoeleka sana kwenye kipindi hicho. 8. Perfect Crispin – Club 10, Clouds FM Perfect ni mtangazaji wa kipindi cha vijana hususan wa sekondari cha Club 10. Ni kipindi maarufu zaidi kwa wanafunzi wa sekondari kuliko vyote nchini na kwa kiasi kikubwa ameendelea kukimudu na kukiendesha kwa ustadi mkubwa mwaka 2013. 9. Jimmy Jamal – Daladala Beat, Magic FM Dala Dala Beat ni miongoni mwa show kongwe kabisa za burudani nchini. Jimmy ni mtangazaji mwenye sauti nzito na mwenye uelewa mkubwa wa muziki wa ndani na nje. Napenda namna anavyofanya interview zake na uchangamfu hewani. 10. King David Kwa wengi, King David ni jina geni kabisa. Lakini kitu kimoja cha uhakika kuhusu jamaa huyu ni kwamba ukimsikiliza lazima utamkubali na kama angekuwa anatangaza redio kubwa, kwa sasa angekuwa akicheza ligi moja na watangazaji wengi hao juu. Ana sauti nzuri na yenye mamlaka, anajua muziki wa ndani na nje na ni mbunifu. Alikuwa mtangazaji wa Uplands FM ya Njombe ambako alikuwa akifanya vipindi kama Bonge la Drive na Uplands FM Top 20 na kwa sasa amehamia kwenye kituo cha redio kipya kiitwacho Kings FM cha Njombe kitakachoanza rasmi matangazo mwakani.
Umaarufu wa Bizzo ulianzia Ebony FM, Iringa ambako alikuwa akifanya show iitwayo The Splash. Kwa sasa Bizzo ambaye jina lake halisi ni Renatus Kiluvya, ni mtangazaji wa kipindi cha Show Time cha Radio Free Africa. Kwa kiasi kikubwa amejitahidi kuliziba pengo la Kidbwoy aliyekuwa amezoeleka sana kwenye kipindi hicho. 8. Perfect Crispin – Club 10, Clouds FM Perfect ni mtangazaji wa kipindi cha vijana hususan wa sekondari cha Club 10. Ni kipindi maarufu zaidi kwa wanafunzi wa sekondari kuliko vyote nchini na kwa kiasi kikubwa ameendelea kukimudu na kukiendesha kwa ustadi mkubwa mwaka 2013. 9. Jimmy Jamal – Daladala Beat, Magic FM Dala Dala Beat ni miongoni mwa show kongwe kabisa za burudani nchini. Jimmy ni mtangazaji mwenye sauti nzito na mwenye uelewa mkubwa wa muziki wa ndani na nje. Napenda namna anavyofanya interview zake na uchangamfu hewani. 10. King David Kwa wengi, King David ni jina geni kabisa. Lakini kitu kimoja cha uhakika kuhusu jamaa huyu ni kwamba ukimsikiliza lazima utamkubali na kama angekuwa anatangaza redio kubwa, kwa sasa angekuwa akicheza ligi moja na watangazaji wengi hao juu. Ana sauti nzuri na yenye mamlaka, anajua muziki wa ndani na nje na ni mbunifu. Alikuwa mtangazaji wa Uplands FM ya Njombe ambako alikuwa akifanya vipindi kama Bonge la Drive na Uplands FM Top 20 na kwa sasa amehamia kwenye kituo cha redio kipya kiitwacho Kings FM cha Njombe kitakachoanza rasmi matangazo mwakani.
No comments:
Post a Comment