Misa ya kitaifa ya wafu kumuaga Hayati Nelson Mandela, inaendelea mjini Johannesburg Afrika Kusini. Rais
wa Marekani Barack Obama na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
watakuwa miongoni mwa viongozi wa dunia watakaohutubia muhadhara huo.
Rais
wa Marekani, Barack Obama na Mke wake wakisoma kitabu cha ratiba ya
misa ya kumuombea rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela
aliyefariki akiwa na umri wa miaka 95.
Mke
wa Marehemu, Graca Machel akiwa kwenye hali ya uzuni wakati wa misa ya
kumuombea marehemu Nelson Mandela aliyekuwa rais wa zamani wa Afrika ya
kusini.
Viongozi hao pia watahutubia wananchi sawa na wajukuu wanne wa Mandela . Maelfu ya watu wamehudhuria misa hiyo katika uwanja wa FNB. Afrika
Kusini imeandaa shughuli mbali mbali za kumuenzi Mandela kabla ya siku
ya kuzikwa kwake nchini Afrika Kusini siku ya Jumapili. Misa ya leo ni moja ya mikusanyiko mikubwa ya viongozi wa kimataifa iliyoshuhudiwa nchini humo katika miaka ya hivi karibuni.
Rais
wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma alipowasili kwenye uwanja First
National Bank (FNB) kwa ajili ya maombezi ya mwili wa rais wa zamani wa
Afrika ya Kusini Mzee Nelson Mandela
Misa hiyo itafanyika katika uwanja ambako Nelson Mandela alionekana kwa mara ya mwisho hadharani. Misa hiyo itaonyeshwa kwenye skrini kubwa nje ya uwanja ili kuzuia msongamano wa watu. Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95 na kwa wengi yeye ni shujaa na mkombozi wa Afrika Kusini
Rais
wa Brazil Dilma Rousseff (kulia) akiwasili kwenye uwanja wa First
National Bank (FNB) kwa ajili ya maombezi ya mwili wa rais wa zamani wa
Afrika ya Kusini Mzee Nelson Mandela
Viongozi wengine Watakaohudhuria misa ya wafu ya Mandela: Watu
wengi wamekaidi hali mbaya ya hewa ambapo mvua kubwa imenyesha huku
wakikusanyika uwanjani humo wakisubiri kwa muda mrefu kabla ya misa hiyo
kuanza muda mfupi uliopita. Waliohudhuria
misa hiyo wamesemekana kuwa wenye furaha wakiimba nyimbo na kutaja jina
la Mandela kwa shangwe unaweza kudhani ni mkutano wa kisiasa.
Mjukuu
wa rais wa zamani, Mandla Mandela akiwa kwenye uwanja wa First
National Bank (FNB) kwa ajili ya maombezi ya mwili wa rais wa zamani wa
Afrika ya Kusini Mzee Nelson Mandela
PICHA NA YAHOO NA HABARI NA BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment