Huenda
ukawa umejiuliza swali hili kwa kipindi kirefu lakini hujawahi kupata
jibu. Kwanini Tanzania, Afrika Kusini na Zambia zinatumia wimbo wa taifa
wenye melody inayofanana?
Enoch Sontonga
Wimbo
huo ulianza kutumika kama wimbo maalum wa hekaheka za ukombozi wa
Afrika na baadaye kuanza kutumiwa kama nyimbo za taifa za nchi tano
barani Afrika, zikiwemo Zambia, Tanzania, Namibia na Zimbabwe baada ya
kupata uhuru.
Zimbabwe
na Namibia zimepata nyimbo zingine za taifa. Wimbo huo kwa sasa
unatumika Tanzania, Zambia na tangu mwaka 1994 kama sehemu ya wimbo wa
taifa wa Afrika Kusini.
Hata
hivyo ikumbukwe kuwa Tanzania ndio ilikuwa nchi ya kwanza kuanza
kuutumia wimbo huo kama wimbo wa taifa 1961 pale ilipokuwa Tanganyika na
kuendelea nao baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964
Tafsiri ya mashairi ya awali yaliyokuwa kwa lugha Xhosa kwenda Kiswahili ilifanya na kundi la watu.
Wimbo
unaotumiwa na Afrika Kusini hata hivyo ni mchanganyiko wa “Nkosi
Sikelel’ iAfrika” na “The Call of South Africa” (unaojulikana kwa lugha
ya Afrikaan kama “Die Stem van Suid Afrika”).
20
April, 1994 ndipo ilipotangazwa kwamba zote Nkosi Sikelel’ iAfrika na
Die Stem ziwe nyimbo za taifa za Afrika Kusini. Wimbo uliounganishwa
ulianza kufanya kazi October, 1997, baada ya maneno ya Kiingereza
yalipoongezwa na wimbo kupangwa upya na Jeanne Rudolph.
No comments:
Post a Comment