RIYAMA amesema kuwa anachukizwa na vitendo vya kimapenzi
vinavyoonyeshwa kwenye filamu nyingi za sasa, ikiwemo mabusu ya staili
ya kulana denda.
Riyama alisema kuwa zamani walikuwa wanapigana
mabusu mashavuni kama ishara ya mapenzi na kusameheana, lakini sasa
wanakula denda kabisa.
“Vitendo hivi ni uchafu wa wazi kwenye jamii, hata
kama kuna namna ambavyo wanafanya lakini bado kuna tatizo, mtazamaji
ambaye ni mtoto, kijana, mzee haelewi hilo, yeye anajua wanapeana denda
kitendo hiki sikipendi,” alisema.
Riyama aliwajia juu wale wote wanaopenda kuigiza
uzungu uliopitiliza kwa kuwa imekuwa ikizua lawama miongoni mwa wadau wa
filamu.
“Hii ni ajira yetu, ni heshima kwa familia zetu,
bado tuna nafasi ya kuifanya iwe bora na ya kuheshimika kuliko kuiga
vitu ambavyo vinafanya ionekane katika mtizamo usio wa kiungwana wakati
waigizaji ni waungwana kama watu wengine lakini matendo ndiyo
yanayotuangusha,”alisema.
Imekuwa ni jambo la kawaida kwa filamu zinazoigizwa nchini kuhusisha vitendo vya aina hiyo licha ya baadhi ya watu kulalamika.
No comments:
Post a Comment