Katika kuadhimisha miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika rais Jakaya Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa 1,475.
Taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Emmanuel
Nchimbi imesema wafungwa watakaonufaika na msamaha huo wa rais ni wale
wagonjwa wa Ukimwi, kifua kikuu na saratani ambao wako kwenye hali
mbaya. Wengine ni
wazee wenye umri zaidi ya miaka 70 walioingia
kifungoni na mimba na wale wenye watoto wachanga na wale wenye ulemavu
wa mwili na akili.
Aidha msamaha
huo wa raia hautawahusu waliohukumiwa kunyongwa au wanaotumikia kifungo
cha maisha, wanaotumikia kifungo kutoka na makaosa ya biashara ra ya
dawa za kulevya , rushwa, wizi na unyang’anyi wa kutumia silaha ,
waliobaka, kunajisi au kulawiti, wezi wa magari na wale waliowapa mimba
wanafunzi.
Wengine ni wale waliofungwa kwa matumizi mabaya ya madaraka
na wale waliowahi kutoroka wakati wa kifungo
No comments:
Post a Comment