Hii chini ni taarifa yake aliyoisambaza kwa vyombo vya habari:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI YA NDUGU ALLY O. CHITANDA
NDG: WANA HABARI:
Kwanza kabisa ninawashukuru kwa kuitika wito wangu.
Jina langu naitwa ALLY OMARY CHITANDA, nimejiunga CHADEMA mwaka 2003 nikitokea NCCR –MAGEUZI.
Nyadhifa nilizowahi kuzishika na kukitumikia Chama ni:-
Kuanzia
mwaka 2004- Mjumbe wa Baraza kuu Taifa nikiwakilisha vijana Bara
niliendelea kuaminiwa na Chama na kupewa kazi nyingine za kukitumikia
Chama, nimewahi kuwa Afisa wa Vijana Makao Makuu, Afisa wa sheria na
Haki za binadamu Makao Makuu, Katibu wa Kamati ya muda ya Baraza la
Vijana Taifa (BAVICHA) kwa sasa ni Mjumbe wa Mkutano Taifa nawakilisha
Nachingwea,Mwenyekiti wa Mkoa wa Lindi tangu tarehe 26/05/2013.Pia ni Afisa Mwandamizi Ofisi ya Katibu Mkuu Makao makuu Dsm.
vile vile kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nikifanya shuhuli ya uandishi wa kumbukumbu za sekretarieti ya chama kama KATIBU WA SEKRETARIETI YA KAMATI KUU.
Hivyo
sasa, pamoja na mambo mengine yapo masuala nyeti na muhimu
ninayoyafahamu na ikibidi kuwaarifu watanzania kwa njia mbali mbali
pindi itakaponihitaji kufanya hivyo.
Ndugu zangu wanahabari,
nimewaita ili kupitia nyinyi niwaambie Watanzania wenzaqngu juu ya hali
ya kisiasa ilivyo hasa ndani ya Chama chetu. Itakumbukwa kuwa tarehe
20-21/11/2013 Kamati kuu ya Chama ilikaa pamoja na mambo mengine
ilifanya maazimio ya kuwavua nafasi za Uongozi ndani ya Chama alikuwa
Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Mhe. ZITTO KABWE na Mjumbe wa Kamati kuu wa kuchaguliwa Mhe. Dr. FITILA MKUMBO, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kwa sababu:-
(a) Mhe. ZITTO KABWE (Mb) alishiriki kusaidia Wabunge watatu wa CCM kupita bila kupingwa kenye Majimbo yao ya Uchaguzi 2010.
(b) Kuandaa mkakati waliouita mabadiliko ya Chama 2013. Mkakati uliolenga kumuwezesha Mhe. Zitto kushinda nafasi ya Uenyekiti wa Chama Taifa endapo angekubali kugombea.
(c) Mhe. Zitto alishindwa
kutimiza majukumu yake ndani ya Chama kwa kutoshiriki pamoja na
Viongozi wenzake kwenye matukio makubwa yaliyokikumba Chama kama:-
(i) Maandamano ya Arusha.
(ii) Operesheni zilzofanyika Morogoro na Iringa nk.
MAAMUZI MENGINE YA UBORESHAJI WA MAKAO:
Ni
kweli kuwa pamoja na mambo mengine Baraza kuu la Chama iliridhia
pendekezo lililetwa kwake na Kamati Kuu kuhusu jambo hili.Na katika
utekelezaji wake Kamati Kuu ya juzi iliridhia kuwa, uteuzi wa
Wakurugenzi watano ambao ni:-
1. Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson.
2. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika (Mb).
3. Mkurugenzi wa Fedha na uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
4. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
5. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.
Uteuzi
huu hauonyeshi sura ya Kitaifa Wakurugenzi wote watano ni Wakristo
kanakwamba CHADEMA hakuna Waislamu wenye uwezo wa kushika nafasi hizo.
Lakini
pia hauzingatii mgawanyo wa kijamii kwa kuwa kati ya kurugenzi hizo
sita wakurugenzi wanne kati yao wanatokea mkoa mmoja wa kilimanjaro
Na uteuzi huu unakwenda sambamba na kuboresha maslahi yao kwa kuongeza posho, -kutoka Tshs. 800,000/= za awali na sasa itakuwa ni kuanziaTshs. 1,500,000-2,500,000/= kwa Mkurugenzi na kutoka Tshs. 6,800,000/= kwa Afisa Mwandamizi na sasa ni Tshs.1,000,000-1,500,000/=.
Pamoja na kwamba uboreshaji uliridhiwa, lakini katika mpango ulioridhiwa na Baraza kuu ni pamoja na kulipa Posho kwa Makatibu wa Wilaya na Mikoa.
Hawa ndio watendaji muhimu katika Ujenzi na Uhai wa Taasisi hii lakini,
hawakuangaliwa wala kuguswa badala yake wanatakiwa kujitolea tu kwa
hali na mali.
Mimi kama nilivyotangulia kusema hapo awali, kuwa
niko kwa kwa miaka 10 sasa na nimeshiriki kwa kiasi kikubwa katika
Ujenzi wa Chama hiki.Sioni sababu ya kutoharakisha kulipa posho ya
Mkatibu wa Wilya na Mikoa pamoja na watendaji wengine na badala yake
tunaharakisha kujilipa posho nono sisi watendaji wa Makao Makuu, wakati
hawa wa ngazi za chini wanamaeneo makubwa ya Kiutendaji na wanafanya
kazi katika mazingira magumu kwa kujitolea hata Ofisi zao wanajitolea
wenyewe.
MAAMUZI YA KAMATI KUU
Ningependa kuwaambia
wanachadema na watanzania kwa ujumla, maamuzi haya ya kamati kuu ya
kuwavua uongozi zitto kabwe na dkt mkumbo ni maamuzi ya kijuha na
yanayowafanya watanzania sasa waangalie mara mbili mbili kama hawa watu
wapo makini na huo ukombozi wanaousema.
Tumekuwa tukiweka
mikakati mbali mbali ya ushindi ili chama kishinde, kwa mfano, kabla
hata ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa arumeru mashariki, wakati tu
ilipobainika anaugua, chama kiliandaa mkakati wa kushinda ubunge wa
jimbo hilo na uchaguzi uliporudiwa mkakati ule ulitumika na kushinda.
Nikiwa
mtendaji wa ofisi ya katibu mkuu, nimeshiriki pamoja na zitto kabwe na
dkt Slaa kupanga mikakati mbali mbali mizuri na mibaya kwa nchi, lakini
hatukuwahi kuitwa wasaliti, wahaini wala sina lolote baya. Ni fedheha
leo mimi kuwa sehemu ya watu wanaomuita zitto kabwe ni msaliti. Siwezi
kuendelea na ujinga huu na sipo tayari tena.
Si dhambi kumuhukumu mtu kwa kuwa anapanga mipango ya kukushinda kwenye uchaguzi, dawa ya mpinzani wako ni kumkabili.
Naomba
nikiri kwamba nikiwa katibu wa sekretarieti tumekuwa tukilazimishwa
mara kadhaa kuwashawishi wajumbe wengi kutowaunga mkono watu wenye
misimamo thabiti ndani ya chama na badala yake tumekuwa tukitumia
rasilimali za chama kuwajenga wajumbe ndio.
Kwa mfano hivi sasa
tunapozungumza, wakati katibu mkuu wa chama anasema mjadala wa zitto
kabwe umefungwa rasmi, amewaagiza wakurugenzi wa chama kuzunguza nchi
nzima kusambaza waraka waliouandaa ukimchafua zitto. Hii si sawa hata
kidogo, si vema kutumia rasilimali za chama kuwanufaisha watu binafsi
kutimiza matakwa yao ya kisiasa.
Nafsi yangu haipo tayari kuendelea kuwa sehemu ya upotoshaji dhidi ya watanzania wenzangu.
Nafsi yangu inanikataza kabisa kuendelea kufumbia macho maovu yanayoendelezwa na chama changu.
Nafsi yangu imechoka kuendelea kushuhudia ubaguzi wa kidini na kikabila unaofanywa wazi wazi na viongozi wa chama changu.
Nafsi
yangu imekataa sasa, haipo tayari tena kuwa kuwadi wa kuwahadaa
Watanzania kuyafikia matarajio tunayowapa ambayo kamwe hayafikiki.
Kwa
kuwa siamini kwamba kuvuliwa nyadhifa kwa zitto kabwe na dkt kitila
mkumbo ni kwa sababu ya waraka wa ushindi, bali ninaamini kuvuliwa kwao
ni kutokana na hofu ya uchaguzi, ubaguzi wa kikabila na kikanda.
Hivyo
basi, nikiwa na akili timamu kabisa, leo tarehe 30.11.2013 nimeamua
kujivua nyadhifa zangu zote nilizokuwa nazo ndani ya chama.
Sioni
tena sababu ya kuendelea kuwa MwanaCHADEMA, sioni tena sababu ya kuwa
mwenyekiti wa CHADEMA MKOA WA LINDI, sioni tena sababu ya kuwa KATIBU WA
SEKRETARIETI YA KAMATI KUU.
Kwa kuwa vipaumbele vya chadema ni
kukijenga chama mikoa ya kaskazini. Basi sisi wananchi wa mkoa wa lindi
tunawatakia kila la heri, na kwamba waendelee kukijenga chama chao huko
huko waliko.
Nashukuru wote ambao nilifanya nao kazi pamoja katika kutekeleza majukumu yangu.
Ahsante Sana
A.O. CHITANDA
0753418510
MWENYEKITI CHADEMA MKOA LINDI
MJUMBE BARAZA KUU TAIFA
KATIBU OFISI YA KATIBU MKUU- SEKRETARIETI
No comments:
Post a Comment