27 December 2013

PICHAZ..Maskini Video Queen Jack Cliff (Mtanzania) Anaswa na Dawa za Kulevya CHINA, Anatia huruma niaje...!

Pichani ni mwanamke huyo wa Kitanzania (akiwa amefunikwa uso) aliyekamatwa na kilo 1.1 za heroin huko Macau. Hapo amepigwa picha na vidonge vyake kwenye press conference huko Macau, Disemba 19, 2013.
Mwanamke wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 amekamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao. Dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na jumla ya vidonge 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720. 
Mwanamke huyo alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne iliyopita. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko China.
Polisi wakichunguza vidonge ambavyo huyu mrembo alikuwa amevimeza.
Ok kwa wale walokuwa wakilalamika 'habari nusu nusu' huyo binti anaitwa Jackie Cliff. ..appeared in Diamondz Nataka Kulewa. Was a runners up or something kwenye Miss Tz huko nyuma.
Waandishi wa habari wakipiga picha vidonge vya heroin alivyokamatwa navyo mremboi huyu wa Kitanzania.
Chanzo cha habari: jamiiforum

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname