27 December 2013

NEWS UPDATES: WATU WATANO WAUAWA KWA KUCHOMWA MOTO BAADA YA KUIBA RAMBIRAMBI GEITA

Watu watano wamekufa kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali kwa tuhuma za kuiba rambirambi ya shilingi elfu 65.

Tukio hilo limetokea mchana huu majira ya saa saba na nusu  katika kitongoji cha Nyantolotolo A nje kidogo ya mji wa Geita.

mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa Mzee Luhemeja alifiwa na mjuukuu wake na baada ya kuisha msiba huo hapo jana watu wote walisambaa wakiwepo pia watuhumiwa  waliouawa hao na kurudi makwao.

Mashuhuda wameongeza kuwa usiku huo watu wanaosadikiwa wanaodaiwa kuwa 8 walifika Nyunbani kwa mzee huyo na kuingia ndani ambapo walimkuta mtoto mdogo na kumpiga kofi baadae wakamfuata mzee wakampiga na kumuonba awapatie fedha kwa usalama wake.

Baada ya kumpiga mzee huyo walifanikiwa kuchukua shilingi elfu 60 zinazodaiwa kuwa ni  pesa za rambirambi zilizotolewa wakati wa msiba baada yam zee huyon kufiwa na mjukuu wake.

Imeelezwa kuwa baada ya kuchukua pesa kwa mzee watuhumiwa hao na kumfata mke wake ambaye jina lakehalijafahamika naye wakampiga na kumuumiza kisha  kuchukua kiasi cha shilingi elfu 5 kisha wakatokomea kusikojulikana.

Baada taarifa kusambaa kuwa kuna uvamizi umetokea jeshi la jadi sungusungu lilianza msako na kufanikiwa kumkamata mmoja wa watuhumiwa akiwa na damu kwenye nguo zake na  kumhoji juu ya tukio hilo, mtuhumiwa aliwataja wenzake mmoja baada ya mwingine na jeshi hilo kuwatia mbaroni wote watano.

Baada ya watuhumiwa kutiwa  mbaroni wananchi wenye hasira kali walianza kuwashushia kipigo
kisha kuwachoma moto hapo hapo huku

mmoja kati ya hao watano akikatwa panga kwenye mguu na kudumbukizwa kwenye kisima na kufia humo humo.

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya wilaya Geita Dkt Adam Sijaona amekiri kupokea miili ya marehemu majira ya saa nane na nusu mchana wa leo na gari la polisi waliofika muda mfupi baada ya tukio wakiwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Geita.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita kamishina msaidizi mwandamizi Leonard Paul amethibitisha kutokea kwa tukio na kuwataja majina yao kuwa ni Juma Patrick Kigara,Marwa,Chacha Kigara,na wawili waliofahamika kwa Eze na Shija na wa tano akiwa hajafahamika jina lake.

Kamanda Paulo amesema tayari watu watatu akiwemo kiongozi wa jeshi la jadi wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi huku jeshi likiendelea kufanya  uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwandishi wa habari hizi kutoka mkoani Geita Valence Robert asilimia kubwa ya wanaumme wamekimbia miji yao kutokana na msako mkali unaofanywa na jeshi la polisi kubaini wahusika wa tukio hilo

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname