27 December 2013

MKE ADAIWA KUMUUA MUMEWE JIJINI DAR

SHETANI anazidi kuuatamia ulimwengu! Mama mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Farida mkazi wa Mburahati jijini Dar, amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kudaiwa kumuua mumewe aliyetajwa kwa jina la Amosi Joseph kwa kumpiga kwa kikombe kichwani, Ijumaa linaidondosha kama ilivyo.
Akisimulia mbele ya gazeti hili mkasa mzima, mtoa habari hii aliyetajwa kuwa dada wa marehemu anayejulikana kwa jina la Khadija, alisema siku ya tukio kaka yake aliamka asubuhi na kumuaga kuwa anakwenda bondeni kwa mkewe (Farida) kwa kuwa walikuwa nyumba tofauti. 
Aliongeza kuwa, muda mfupi baada ya kaka yake kuondoka nyumbani hapo, wifi yake (Farida) alifika nyumbani hapo na kumwambia kuwa kaka yake ameumia sana aende akamuone. 
“Mimi nilimshauri ampeleke hospitali tu nikidhani ameumia kidogo, kwa sababu wamekuwa na kawaida ya kupigana mara kwa mara na tulishawaonya. Wifi aliondoka na mimi nikaendelea na shughuli zangu
 “Muda mfupi, uliingia ujumbe kwenye simu yangu ya mkononi ukisomeka kuwa kaka yangu alikuwa amefariki dunia huku ujumbe huo ukinionya kutolia ili nisimshitue mama,” alisema Khadija. SOMA ZAIDI HAPA

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname