27 December 2013

LADY JAY DEE AWEKA WAZI NDOTO ZAKE ZA KUPIGA COLABO NA DR DRE NA USHER


clip_image001Tunaendelea kuzihesabu siku kadhaa kuikamilisha mbio ya kuumaliza mwaka 2013 Mungu akipenda huku mengi yakiwa yamekamilika na mengine yakiwa pending. 
Binti Komando, Anaconda, Lady Jay Dee bado hajakamilisha mpango wa kuuweka wazi wosia wake, lakini hivi karibuni watanzania na wadau wa muziki wanaweza kuushuhudia wosia huo kabla hatujauanza mwaka 2014. 


Hii inatokana na tweet ya Jide ya December 18,2013.clip_image002 
Katika hatua nyingine, Yahaya hit maker ameweka wazi moja kati ya ndoto ambazo anatamani sana kuzitimiza ikiwa ni pamoja na kukutana na daktari wa midundo duniani ‘Dr. Dre’, na mkali wa R&B Usher Raymond. 
Jide ameandika kwenye blog yake: 
“Kati ya NDOTO zangu mbili kubwa zilizobakia hapa duniani ni kukutana na watu hawa wawili Dr. Dre na Usher Raymond 2013 hiyoooo inayoyoma ndoto imekuwa ndoto, hebu tusaidiane kusali tujaribu tena 2014.”

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname