31 December 2013

KWA NINI MSICHANA WA KAZI AKUCHUKULIE MUME WAKO-2

ASALAAM aleiykhum/Bwana Yesu asifiwe Bila shaka wasomaji wa safu hii hamjambo na mnaendelea vema na shughuli za ujenzi wa taifa.
Kwa wale wagonjwa, nawaombea dua mpone haraka na kuuanza mwaka 2014 kwa furaha. Leo tunaendelea na mada yetu ya wiki iliyopita, nilipata ujumbe mwingi kwa njia ya simu kutoka kwa wasichana wa kazi na akina baba wenye nyumba wakiwa na mawazo tofauti.


Haya ndio makosa wayafanyayo wanawake wenzangu
Wanawake wenzangu, mambo mengine kiukweli huwa tunajitakia, nakuomba usome maelezo haya ya msichana huyu wa kazi aliyonitumia baada ya makala ya wiki iliyopita:

“Hapo umegonga ikulu Bi Chau, mimi pia ni ‘house girl’ , bosi wangu (mke) anategemea nisafishe chumba chake cha kulala , nitandike kitanda anacholala na mume wake, niwafulie nguo zao za kuvaa mpaka za ndani, maji niwapelekee bafuni, hiyo haitoshi hata chakula na nawapikia, usiku namfungulia mimi mumewe, Je, yeye ni mke mwenzangu?

“Nikijilegeza kwa mume wake, namchukua kikwelikweli, yeye (mke) anashindwa kumtimizia mambo mengi, akinipata atamsahau milele…”
Hii ni sehemu ya ujumbe ambao nimetumiwa na mmoja wa wasichana wa kazi za ndani, nadhani mnaona jinsi wanawake wenzetu wanavyojitakia kunyang’anywa waume.

Ningemjua huyo bosi wake ningemshukia na kumuuliza kwa nini anafanya hivyo? Mwanamke hajui soksi wala kitambaa cha mumewe kiko wapi. Utasikia akiuliza; Dada hivi zile soksi ulizofua juzi za baba ziko wapi?

Niwaulizeni wasomaji, nani alaumiwe kwa hilo? Mtabaki kusema eti mume amehamishia penzi kwa msichana wa kazi, kapewa limbwata! Ukweli ni kwamba wake wengi huwa wamelikoroga mwenyewe.
Wewe umestarehe unasubiri sita kwa sita tu, jamani fanyeni ubunifu wa lifestyle!

Meseji ingine ilitoka kwa mwanaume ukiisoma kama uliachika unaweza kung’amua kwa nini mumeo alikuacha wewe aliyekutolea mahari kwenu na kumchukua msichana wa kazi kirahisi akamuingiza chumbani kwenu, aliandika hivi:

“Bi Chau mimi ni mwanaume ninayejiweza, nina mke ambaye naye anafanya kazi, kiukweli nikipendeza kazini aliyenipendezesha kimavazi ni msichana wa kazi.
“Msichana wa kazi ndiye hufua na kunyoosha nguo zangu na kujua ipi imechanika, nakumbuka siku moja nilitaka kuvaa shati likawa halina kifungo,  mke wangu alikuwa anajiandaa kwenda kazini nikamwambia, eti akamuita dada wa kazi na kumuamuru atafute uzi, anishonee kifungo.

“Wakati huo yeye alikuwa anakunywa chai, Bi Chau lilinikera sana hilo tukio na siku hiyo jioni nikamsema sana lakini pia hakukiri wala kuona kosa lake,…” aliandika msomaji huyo wa kiume.
Ujumbe huu unasikitisha, heshimu ndoa yako la sivyo utamaliza waganga wote kumbe ubovu unao mwenyewe. Halooooo!!!!!

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname