Balaa tupu!: Wachezaji wa Raja Casablanca wakiwa wamemzunguka Ronaldinho kutaka viatu vyake
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
BAADA
ya kutolewa katika mchezo wa nusu fainali wa klabu Bingwa ya Dunia ya
FIFA, inawezekana Ronaldinho alikuwa anataka kurejea kwenye chumba cha
kubadilishia nguo cha klabu yake ya Atletico Mineiro ili kujiliwaza
kufuatia kula kipigo.
Lakini
mambo yalikuwa tofauti baada ya kujikuta akikaa uwanjani kutokana na
wachezaji wa Casablanca kumvamia wakiomba viatu vyake vya Nike.
Wamorocco
hao waliendeleza ndoto zao za kuchukua ubingwa wakiwa wenyeji baada ya
ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Wabrazil jana, huku Ronaldinho akifunga
bao zuri kwa njia ya adhabu na kufufua matumaini ya kutwaa ubingwa kama
alivyofanya mwaka 2006 akiwa na Barcelona.
Raha tu: wachezaji wa Casablanca wakifurahia ushindi
Mouchine
Iajour aliifungia timu yake ya Raja bao la kuongoza kabla ya
Ronaldinho kusawazisha, lakini Mouhcine Moutouali aliandika bao la
pili dakika ya 84 kwa njia ya penati na Vivien Madibe aliwazamisha
Wabrazil hao kwa kuandika bao la tatu .
Raja sasa itakumbana na mabingwa Ulaya, FC Bayern Munich siku ya jumamosi katika mchezo wa Fainali mjini Marakech
Wachezaji wa Raja Casablanca wakishangilia ushindi wao wa 3-1 dhidi ya Atletico Mineirokatika dimba la Marakech
Ushangiliaji: Wamorocco watavaana na Bayern Munich katika mchezo wa fainali wa klabu bingwa ya Dunia ya FIFA
Haamini:
Ronaldinho alifunga, lakini alishindwa kupia klabu yake ushindi,
angeshinda angekutana na kocha wa zamani wa Barca, Pep Guardiola
No comments:
Post a Comment