Msanii wa kundi La Last Warning, Inno Mtoa Lock ameingia kwenye tuhuma
kubwa kutoka kanda ya kaskazini baada ya kuachia ngoma yake wiki mbili zilizopita inayokwenda kwa jina la nilivyomkuta dar ambayo amemshirikisha jamaa toka kundi la jambo squad ambaye ni jogoo kichaa a.k.a ordinary na kazi ikiwa imetengenezwa pale Noiz Mekah ,producer akiwa Dx kuwa huo wimbo ni dongo la moja kwa moja kwa msanii Joh Makini Mwamba Wa Kaskazini .
akihojiwa katika interview ya radio moshi fm katika kipindi cha the base show ambacho huwa kinaanza saa saba hadi saa kumi kamili jioni , mtoa lock alikumbana na wakati mgumu sana baada ya wadau na wasikilizaji wa hiyo radio waliotaka kujua ukweli kutoka kwake kuhusiana na habari zilizozagaa mitaani kuhusiana na ngoma hiyo kuwa ni dongo kwa Joh Makini Mwamba Wa Kaskazini .
wasikilizaji walitaka ufafanuzi juu ya ngoma hiyo na madai kuwa ni kweli ni dongo kwa msanii Joh Makini au ni habari tu. msanii huyo hata hivyo alionekana kushtushwa na swali hilo na kushindwa kutolea ufafanuzi wa kina juu ya wimbo huo na badala yake alisema ni wimbo tu ambao upo hivyo na wala si kweli kuwa amempiga dongo Joh Makini.
Joh Makini
hata hivyo blog ya DJMwanga.com ilipoamua kumtafuta Mtoa Lock juu ya kile kilichojiri katika interview yake hiyo, alisema yeye mwenyewe hajui kinachoendelea juu ya tuhuma hizo na alishangazwa sana na maswali hayo ambayo yalikuja mfululizo katika interview yake ambayo yalimtaka atolee ufafanuzi juu ya madai hayo.
"patty katika kitu ambacho kilinishtua na kunishangaza ni juu ya maswali yaliyokuja mfululizo yakituhumu kuwa wimbo wangu wa “nilivyomkuta dar”, ambao nimeuachia hivi karibuni kabla ya sikukuu ya christmass kuwa nimemlenga Joh Makini Mwamba Wa Kaskazini ,kitu ambacho sio kweli, nani idea tu ya wimbo na style zetu kama last warning."alisema Mtoa Lock.
wimbo wa Nilivyomkuta Dar, ambao una wiki ya pili tangu uachiwe umekuwa gumzo kanda ya kaskazini naukizidi kuwa na tuhuma kwa msanii wa ngoma hiyo Inno Mtoa Lock,kwamba amemuimba Joh Makini msanii ambaye anafanya poa sana katika gemu la hip hop ambapo anatoka kundi la weusi.
baadhi ya mashairi yaliyopo katika ngoma hiyo nilivyomkuta dar, kachaa wa kitaa
alikuwa gangstar aisee, sasa pang'ang'a balaa,
alikuwa ananyoa dongo,sahivi nywele kafuga,
midosho ya kibongo,hana modo za kichuga,
katekwa na mabishoo,katema pigo za huku
hachezi ngaleloo ye ni bingwa wa viduku..................
anasema anaswaga ,wazazi amewatupaga , jiji limemtekaga,
anapenda vizaga,
anasema arusha siji kula viporo.
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
•
No comments:
Post a Comment