Godzilla na Diamond kuachia collabo mwakani......hii itakua zaid ya muziki gani...
Ni nadra sana kwa Diamond Platnumz kufanya collabo na tena
na msanii wa Hip Hop. Mwaka huu hitmaker huyo wa ‘My Number One’
alishirikishwa na Nay wa Mitego kwenye ‘Muziki Gani’ na kushuhudia
mafanikio makubwa kwa Nay ambayo ni pamoja na kuongeza mashabiki zaidi
na kupata show nyingi zilizomfanya kuwa miongoni mwa wasanii walioingiza
mkwanja mwingi mwaka huu.
Sasa ni zamu ya Godzilla kupata neema za Diamond Platnumz, kipenzi
cha wengi. Wakali hao watasikika kwenye ngoma ya pamoja iliyofanyika MJ
Records na ambayo itatoka mwaka 2014.
“Zilla &diamond platinum&za chaa&marco chalii . ..on the
same page ,whts my name jan ....see you 2014,” ametweet Godzilla jana.
Hakuna wasiwasi kuwa hiyo itakuwa hit ya mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment