Msanii wa bongo fleva Linex Sunday
Mjeda amefanya collabo na wasanii wenzake wanaouwakilisha mkoa wa Kigoma
Ommy Dimpoz pamoja na Recho katika wimbo wake mpya aliomaliza kuurekodi
jana.
Akizungumza na Bongo5 leo, Linex
amesema wimbo huo utakuwa ni wa tofauti na nyimbo ambazo zimezoeleka kwa
Watanzania na kuongeza kuwa katika wimbo huo mzee wa Tupogo Dimpoz
ameimba kwa kuchanganya na lugha ya Kiha.
“Hiyo ngoma jana ndiyo tumemaliza mimi
Dimpoz na Recho, imefanywa na Fundi Samweli pamoja na Tudd Thomas na
ngoma inaitwa INGO, Ommy kaimba Kiha hatariiii” Amesema Linex.
Akielezea maana ya Ingo, Linex amesema
“Ni Kiha na maana yake ni Njoo, but ni neno linalotumika kwa makabila
mengi East Africa kama Rwanda, Burundi na UG”.
Katika wimbo huo Linex amesema yeye na
Ommy wamegawana verse moja moja, huku chorus akisimama mwenyewe na
vionjo vya sauti tamu ya Recho vimepita kwa mbali.
Kuhusu mipango ya video ya wimbo huo
Sunday Mjeda aka V.O.A amesema tayari amesaini mkataba na Samaki Samaki
ambao ndio watakaosimamia video hiyo.
“Pia nimesaini contract na Samaki
Samaki Fleva juzi kwaajili ya kushoot video kubwa, so wao ndiyo watakuwa
wasimamizi wa video ya ‘Ingo’.
Linex ameongeza kuwa anatarajia kuutoa wimbo huo January 2014.
Credit-Bongo5
No comments:
Post a Comment