Linah Sanga maarufu kama Lina kutoka jumba la vipaji Tanzania (THT) anayetamba sasa na ngoma yake ya ‘Tumetoka Mbali’, ameamua kuwachana wale wote wanaomfuatilia nje ya muziki. Linah amekuwa ni miongoni mwa wasanii wa kike wanaovaa nguo fupi sana wawapo kwenye showz zao kitu kinachopelekea wengi kuwa na maswali na mtazamo hasi juu ya uvaaji huo. Akiongea na E-Newz ya EATV, Linah amesema kuwa mtindo wake wa mavazi unazingatia sehemu anayokuwepo na ushauri anaoupata kutoka kwa watu wake wakaribu baada ya kujadiliana nao na kuona kuwa atapendeza na atavutia zaidi akivaa hivyo. “Wakati mwingine nafikiria kuwa huwezi kumridhisha kila binadamu, kuna watu wanapenda Linah avae hivi na wengine avae vile. Sasa kuna wakati unafika inabidi inafikia hatua unaamua kwamba mimi ni wa hivi na utaelewa kuwa mimi ni wa hivi kama hutaki basi as long as unachotakiwa kunifuatilia mimi ni kazi yangu ninayofanya either unafurahi na kazi yangu au haufurahi.” – Linah.
No comments:
Post a Comment