11 December 2013

DUH..!"Ukweli Nitaendelea kuusema Siku zote kwamba Diamond hajui Ku.. "....Baby Madaha azidi kumponda Diamond

Kwenye hizi siku mbili tatu headlines za Magazeti, blogs, website na vyanzo vingine vya habari zimemilikiwa pia na habari kuhusu Diamond Platnumz na Baby Madaha kuhusu kurushiana maneno baada ya kauli ya kwanza ya Baby.

Madaha amezungumza ya moyoni na mwandishi wetu baada ya kusambaa kwa taarifa hizi na kufafanua kwamba ‘kiukweli ni kwamba hakuna ugomvi wowote labda ni yeye anaukuza ama ni nini, mimi sina ugomvi nae wala sitaki… nilichoongea ni ukweli kwamba alikua hajui muziki, uwezo wake huwezi kuulinganisha na Barnaba au Ali Kiba, nilitoa maoni yangu so haina haja ya kusema ni chuki’ 
‘Ukweli siku zote watu wanauogopa so sijali atajibu nini kwa sababu niko tayari kumjibu na nitasimamia kwenye point yangu na yeye kama ataongea aongee, muziki hauna Mungu mtu wa kusema kwamba asiambiwe kitu chochote hata kama anakosea, hata kama anaiba mashairi ya watu wengine asiambiwe? hata kama wimbo wake sio mzuri asiambiwe? tunahitaji changamoto kwenye muziki’ – Madaha Kwa kumalizia, 
Madaha anasema ‘aumize kichwa kama wenzake na aweze kufanya muziki vizuri ambao hautategemea kiki kupitia skendo za mapenzi, asijiweke sana kweye skendo ili watu waelewe uwezo wake binafsi Diamond kama Diamond, so hiyo haikua beef… ni ukweli na ukweli uauma na kuogopwa, ndio maana akareact’

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname