Gabriel Kimolo |
Katika hali ya kuonyesha CCM hapako shwari leo mkuu wa Wilaya
Gabriel Kimolo amevua gamba na kuvaa Gwanda hii leo ni kwenye Kongamano
linaloendelea muda huu katika hotel ya Land mark ambapo wangeni rasmi ni Tundu
Lisu, Mnyika, Lema, Msigwa, Heche na Kilewo.
HABARI KAMILI
Kwa mujibu wa Bw. Kimolo, miongoni mwa sababu za kujiuzulu kwake
ni pamoja na kitendo cha yeye kukashifiwa na baadhi ya wafanyibiashara wanunuzi
wa kahawa Wilayani hapo, ambao walifikia hatua ya kumtamkia kuwa hawawezi
kuongea na "mbwa, bali na mfuga mbwa", wakimaanisha hawawezi kuongea
naye bali Waziri Maghembe ambaye inadaiwa alikuwa akiwakumbatia.
“Nimechoshwa na kejeli na mizengwe dhidi ya serikali.
Wafanyibiashara wanadiriki kusema kuwa hawako tayari kuzungumza na mbwa bali
wanazungumza na mwenye mbwa. Siwezi kufanya kazi katika mazingira ya aina hii.
Wananchi waelewe hivyo. Nitabakia kuwa raia mwema na mwananchi wa kawaida kama
wengine” alisema Bw. Kimolo.
Kimolo, ambaye anakuwa kiongozi wa kwanza wa Wilaya kuachia
ngazi katika kipindi cha miaka 20, ya utawala wa CCM, amesema kuwa amekuwa
akikosa Ushirikiano na Wizara ya Kilimo kwa ujumla juu ya msimamo wake wa
kupinga ununuzi wa kahawa mbivu (Red Cherry), kama ambavyo imekuwa ikifanywa na
baadhi ya wafanyibiashara wanaopata ridhaa toka Wizarani.
Januari 7 mwaka huu, Waziri Maghembe, alikutana na baadhi ya
wakulima na wadau wa zao la kahawa ambapo msimamo wa Serikali ulieleza kuwa
hawako tayari kuendelea kuwaona wakulima wakiuza kahawa mbichi kwa wachuuzi hao
hali ambayo Bw. Kimolo amesema ilisababisha yeye kuonekana kutothaminiwa
msimamo wake na Serikali ya Wilaya na ya Mkoa.
Kadhalika katika maelezo yake ya kujiuzulu, amesema kuwa kwa mujibu
wa utaratibu wa uteuzi unaofanywa na Rais, yeye uteuzi wake ulianza mwaka 2006,
na kukoma mwaka 2010 ambapo hadi sasa hakuna uteuzi mpya uliofanywa na Rais
jambo ambalo linamfanya ashindwe kupanga mikakati ya kazi kwa maendeleo ya
Wilaya yake.
Amesema kuwa, hivi sasa ni mwaka mmoja na nusu amekuwa akifanya
kazi kwa matukio ya dharura na maagizo toka juu na hivyo kumfanya aonekane
kutowajibika vilivyo katika nafasi yake na kwamba ameamua kujiuzulu akiamini
kuwa uamuzi wake utalinda heshima yake.
Aidha, inaelezwa kuwa Bw. Kimolo amekuwa ni mtu wa karibu sana
na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na kwamba kitendo chake cha kujiuzulu kina
baraka kutoka kwa kiongozi huyo aliyewahi kuwa Waziri Mkuu kablda ya kujiuzulu,
ambapo katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni Wilayani Momba katika mji
mdogo wa Tunduma, aliteta naye jambo muhimu.
Hata hivyo, tetesi za kutokuwemo katika uteuzi ujao zinaelezwa
kuwa ni moja ya sababu zinazomfanya mkuu huyi kuachia ngazi mapema ili
kujijengea mazingira ya maandalizi ya kuikubali hali hiyo kabla haijatokea
wakati wa uteuzi ambao unatarajiwa kufanywa na Rais wakati wowote kuanzia sasa.
Akasema kumekuwa na baadhi ya viongozi wababaishaji na
kusababisha serikali ionekane inashindwa kuwatumikia vyema wananchi na sasa
yeye ameamua kuachia ngazi na anakwenda kushughulika na mambo yake binafsi.
Alipotakiwa kueleza kama dhamira yake imejikita zaidi katika
siasa, amesema kuwa wakati ukifika kuingia katika mchakato wa kisiasa atafanya
hivyo kwakuwa yeye kama mtu yeyote ana uamuzi wake na katiba inamruhusu kufanya
hivyo.
Amesema kuwa, tayari amemuandikia barua Rais, Waziri Mkuu na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuwajulisha hilo na kwamba huo ni uamuzi wake binafsi na jibu lolote halitabadili uamuzi wake huo.
No comments:
Post a Comment