02 December 2013

BONGO MOVIE IMENIFANYA NIONEKANE CHANGUDOA"....AUNT LULU




MSANII wa filamu na ambaye pia aliwahi kuwa mtangazaji wa TVAunty Lulu, amesema kuwa anajuta ni kwa nini alishawishika kuigia kwenye tasnia hiyo ya filamu kwani ni bora angeendelea na kazi yake ya awali, kwani huko kumemfanya aonekane kama changundoa wakati hayuko hivyo.

Tasnia ya filamu imekuwa ikiwaharibu vijana wengi hasa wakike wanaopenda kufanya kazi hiyo na mwisho wa siku wanaonekana kama wamepoteza muelekeo wa maisha, kutokana na anasa zilizopo ndani ya tasnia hiyo.

Aunty alisema kuwa awali kabisa alipenda kufanya kazi hiyo lakini kadri siku zinavyokwenda mbele anajiona wazi kuwa amebandilika na amekauwa na tabia chafu ambazo hazina mfano.

Alidai kuwa inawezekana hakujua namna ya kujipanga pindi alipokuwa anaigia kwenye tasnia hiyo, lakini sasa anaona wazi kuwa tayari ameshazama kwenye shimo na kutokana kwake ni vigumu kwani hayo ya sasa ndiyo maisha aliyozoea.

“Awali sikuwa hivi asa sijui hii ni kwa sababu ya kuingia kwenye filamu au vipi, lakini kuna matukio mengine nimeyafanya ambayo kwa kweli si mfano wa kuigwa,”alisema.
​ 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname