Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union Steven Mnguto timu yenye
makao yake makuu pale Tanga ametoa taarifa zinazomhusu mwanasoka Haruna
Moshi’Boban’ kuhusu mkataba wao na Boban.
Coastal Union wamesema hawatomuongezea mkataba mshambuliaji Haruna Moshi ‘Boban’ kutokana na kuwa na utovu wa nidhamu.
Steven Mnguto alisema mpaka sasa mshambuliaji huyo hajaripoti kambini kuanza mazoezi na wenzake na hajatoa taarifa yoyote.
Mnguto ameongeza kwa kusema kuwa kwa tabia aliyoionyesha ni
ngumu kumuongeza mkataba mshambuliaji huyo aliyebakiza miezi sita tu
katika mkataba wake unaomalizika mwishoni mwa msimu huu.
Kutokana na kutojiunga na kikosi hicho mpaka sasa,Boban
atakatwa mshahara wake wa mwezi huu kwa kuwa hajaufanyia kazi yoyote
tokea alipotakiwa kujiunga na wenzake tarehe 1 Desemba mwaka huu,mbali
na Boban adhabu ya namna hiyo pia itamkuta kiungo Jerry Santo ambaye ni
raia wa Kenya kutokana na kutotoa sababu zozote za kuchelewa kujiunga na
wenzake kambini.
‘Ni bora tukapandisha vijana wetu wa U20 kwa kuwa tunajua
watatusaidia na wana nidhamu ya hali ya juu kuliko hawa ambao ni wazoefu
lakini wanatusumbua upande huo’.
‘Hatuwezi kumuongeza mkataba mtu ambaye tunaona kabisa nidhamu
yake haituridhishi kama timu na hajatoa hata taarifa yoyote. Wa nini
mtu kama huyo? Sisi tunaangalia maslahi ya timu ili ifanye vizuri’. .
Kwenye kumbukumbu Boban aliwahi kuondolewa kwenye kikosi cha
timu ya Simba ambacho alikuwa amekitumikia kwa muda mrefu kutokana
sababu za kiutovu wa nidhamu.
No comments:
Post a Comment