MJANE
wa Msanii wa filam nchini (Bongo Muvi) Marehemu Juma Kilowoko (Sajuki)
Wastara Sajuki, amesema kwamba hana mpango wa kuingia katika mahusiano
ya mapenzi kwa sasa. Wastara ametoa kauli hiyo wakati kukiwa na uvumi
kwamba star huyo wa filamu nchini,anamahusiano na msanii mwenzake, Bond
Bin Suleiman.
Wakati Wastara akitoa kauli hiyo,watu mbalimbali
akiwemo mwanamke aliyewahi kukimbia penzi la jemba hilo, Lulu Semagongo
maarufu kwa jina la (Anti Lulu), akidai kwamba jamaa anatabia ya kula
nyuma na mbele tena kwa kulazisha na wakati mwingine anatumia hata dawa
za kelevya kwa kumpa mwanamke, ili atimize hazma yake.
Akizungumza na
Habarimpya.com Anti Lulu alisema kwamba wakati akiwa kwenye mapenzi na
Bond alishindwa kuvumilia ujinga wake na akalazimika kujiondokea kwa
sababu si mwanaume mwenye maadili ya mapenzi.
"Huyo
jamaa ni mbaya hafai hata kidogo mimi namwonea huruma sana Wastara
maskini, asiposikilisha ushauri huu ataendelea kufanyishwa mapenzi sana
kinyume na maumbele yake"alisema Anti Lulu na kuonge:;
"Minaona
anampango wa kujichafualia sifa yake, najua watu wanaweza kusema kwamba
nina mharibia, lakini ukweli ni kwamba jamaa nilimuacha kutokana na
tabia hiyo, kitambo hivyo siwezi kuwa na wivu na Wastara, ila
ninamshauri awe makini na huyo jamaa kwani ni nomaa sana mwanzo ukimuona
utadhani kuwa ni mtu, lakini ukishaa kolea kwake utakoma, na kama
anabisha asubiri kuona matokeo yake"alisema Anti Lulu kwa kujiamini.
Hata
hivyo Wastara pamoja na jemba lake wamekuwa wakinukuliwa katika
mitandao mbalimbali wakikana kuwa na mahusiano ya mapenzi, zaidi ya
mahusiano ya kazi kwani hivi sasa wako katika hatua za mwisho za kuandaa
filamu yao mpya, itakayojulikana kwa jina la 'Uaminifu Dhaifu' "sina
mahusiano na Bond zaidi ya kikazi tu na zile picha zote ambazo unaziona
ni wakati tupo location, tukiandaa filamu yake inayoitwa Uaminifu
Dhaifu, huo ndiyo ukweli, bora mume wangu angekuwepo haya yote
yasingetokea"alisema Wastars.
Naye Bond kwa uapnde wake alisema kwamba Anti Lulu ni muongo sana,"Sio
kweli ni picha za kazi tu ambazo hata wewe nilikutumia magazeti
yanazigeuza, Lulu achana nae anatafuta kuandikwa, tulishachana kitambo
wala hatuna mawasiliano"alisema Band.
SOURCE-Habarimpya
No comments:
Post a Comment