- Mimi nikiwa Mwana CCM na Kiongozi pia
wa CCM ngazi ya Taifa na Blogger, naomba kusimama mbele ya Mheshimiwa
Mbunge Kapuya na Taifa zima la Tanzania pamoja na wasomaji wangu wote wa
Blog na meble ya Mungu, kukubali makosa na kuomba radhi, kwake na kwa
Mungu wangu zaidi. Mimi ni mmoja wa watu wa kwanza kuamini hadithi
iliyojitokeza hivi karibuni kwamba Mheshimiwa Kapuya amembaka na
kumuambukiza Ukimwi na kutishia kumuua msichana wa miaka 14.
- Leo ninaomba kusimama hapa na kusema
kwamba hii habari ni uongo na ni uzushi wa hali ya juu sana
uliotengeenzwa na msichana mzoefu wa uzushi ambaye kwanza si kweli
kwamba ni Mwanafunzi, pili ni Mtumzima mwenye mtoto tayari hata kabla
hajakutana na Mh. Kapuya, pia ni muongo na mzushi mzoefu aliyewahi
kuwadanganya pamoja na Mkurugenzi wa CRDB Bank, pamoja na kuidanganya
TAMWA ambayo iliishia kumuripoti polisi na kuishia kwake kukaa rumande
Segerea kwa muda mrefu sana.
- Kwa nini niliaiamini hii hadithi ni
kwamba kuna siku mimi binafsi tulikuwa tumekaa faragha na Viongozi
wengine Watatu wakubwa wa Taifa ambapo mbunge mmoja aliyedai kuijua kwa
undani hii hadithi na kuhusiaka nayo, alianza kutuelezea hii hadithi kwa
kutmia details kubwa kubwa sana, binafsi nilikuwa ninamuamini sana yule
mbunge mpaka leo nilipothibitisha kwa 100% kwamba hii hadithi haiko
sawa either na yeye ni muongo wa makusudi mwenye nia mbaya na Mh. Kapuya
au na yeye alidanganywa na huyu msichana, ambaye jina lake kamili ni
Hamida as opposed na majina mengi ya uongo ambayo amekuwa akiyatumia
kudanganyia watu.
- Ninaomba kuwa wa kwanza kubeba huu
msalaba, najua kwamba sio rahisi kueleweka na wengi ambao
tulishamuhukumu Mh. Kapuya, lakini ukweli ni kwamba ni hadithi ya
kutunga iliyoutngwa na msichana mmoja aliyebobea katika uzushi na uongo
wa hali ya juu sana. Majuzi Waziri mmoja ninayemuamini sana katika
Serikali ya sasa alinishitua kwamba hii hadithi ni ya uongo niiifuatilie
tena, lakini sikuamuamini mpaka leo asubuhi sana nilipopigia sim na
gazeti moja maarufu sana la Udaku, walioniambia kwamba hii habari si ya
kweli na kwamba wanaye huyu msichana pale ofisini kwao, toka asubuhi
mpaka sasa nimekuwa kwenye uhakiki wa hii ishu, na sasa ninasema wazi na
tena kwamba:-
NINAMUOMBA RADHI SANA MH. KAPUYA NA NI
MATUMAINI YANGU MAKUBWA SANA KWAMBA WALE WOTE TULIOHUSIKA NA KUMHUKUMU
TUTAKUBALI MAPUNGUFU YETU KAMA WANADAMU NA KUMUUNGAMIA CHINI MUNGU WETU,
NI KWELI MH. KAPUYA ALIKUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA HUYU BINTI
LAKINI YA HIARI SIO KAMA ILIYOELEZWA NA SI KWELI KWAMBA HUYU BINTI NI
MWANAFUNZI, HAPANA ANA MTOTO TAYARI NA PIA ALISHAWAHI KULIDANGANYA JESHI
LA POLISI HUKO NYUMA.
- Wale wote tunahusika na media
tujifunze tena na hili fundisho, tujitahidi kuwa waadilifu na kufanya
utafiti wa kina kabla ya kuruka na hadithi nzito kama hii ambayo inaweza
kummaliza mwananchi mwenzetu, au kiongozi bila sababu za msingi wala
ukweli.
- AGAIN NI MATUMAINI YANGU KWAMBA WALE
TULIOHUSIKA NA KUMHUKUMU MHESHIMIWA KAPUYA, TUTAJITOKEZA TENA IN THE
PUBLIC NA KUMUOMBA RADHI NA MSAMAHA.
- MUNGU IBARIKI TANZANIA NA KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!
WILLIAM MALECELA

No comments:
Post a Comment