04 November 2013

WAMBURA AUNGURUMA BAADA YA UTEUZI WAKE, AWAOMBA WADAU WOTE KUTOA USHIKIRIANO KATIKA MAJUKUMU YAKE, BADO YEYE NI AFISA HABARI WA TFF!!

wambura
Na Baraka Mpenja  wa Fullshangwe, Dar es salaam
MUDA mfupi baada ya Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kumteua Bw. Boniface Wambura kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Uteuzi ambao ni kuanzia jana Novemba 2 mwaka huu, kaimu katibu mkuu huyo amesema yeye bado ni Afisa habari na ana kaimu nafasi hiyo ya mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za TFF.
Akizungumza na mtandao huu mchana huu, Afisa habari na kaimu katibu mkuu huyo mpwa wa TFF,  Boniface Wambura, amekiri kukabiliwa na majukumu makubwa zaidi, lakini amesema kwanini ameteuliwa katika nafasi hiyo, Rais Jamal Malinzi ndiye anaweza kueleza ni taraibu gani zimetumika.

“Cha msingi ni kwamba, nahitaji ushirkiano kutoka wa wadau wote wa soka ili kufika mbali, hapa tulipofika si haba, lakini tunahitaji kufika mbali zaidi”. Alisema Wambura.
Wambura alisema kiukweli majukumu yameongezeka kutoka nafasi yake ya Afisa habari ambayo anaikalia mpaka sasa na sasa kaimu katibu mkuu, ila ameendelea kusisitiza kuwa ushirikiano wa viongozi wote na wadau itakuwa njia sahihi kwake yeye kutekeleza majukumu yake.
Pia amesema taarifa zinazotolewa na mitandao mbalimbali kuwa kuna baadhi ya watu wameondolewa katika nyadhifa zao, Wambura amesema wao hawafanyi kazi kwa uvumi, kama ingekuwa hivyo basi taarifa kutoka kwa Rais Malinzi ingetolewa.
“Kwa sasa yanayozungumzwa ni uvumi, hakuna taarifa yoyote kama kumekuwepo na mabadiliko, lakini kama kuna watu watabadilishwa nafasi zao, basi taarifa kwa Umma itatolewa”. Aliongeza Wambura.
Katika taarifa iliyotolewa leo na TFF aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ameagizwa aende likizo ya malipo hadi atakapomaliza mkataba wake.
Kamati ya Utendaji inaviomba vilabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama shiriki na wadau wote kumpa ushirikiano Bw. Boniface Wambura katika utekelezaji wa majukumu yake.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname