Msanii wa filamu nchini, Steve Nyerere amesema amepata mwaliko wa
kwenda kuhojiwa na shirika la habari la Uingereza, BBC kutokana na
kufanya filamu za kumuenzi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere.
Steve alisema anatarajia kwenda kufanya
show London mapema mwakani pamoja na kuhudhuria mwaliko wake BBC.
“Nipepata bahati ya mwaliko mzuri wakualikwa na kituo cha BBC
London,kama Steve Nyerere ninayemuenzi Nyerere katika filamu,nadhani
mwezi wa kwanza Mungu akinibariki nitaenda,” alisema Steve.
“Kuna kampuni ambayo inanisimamia kazi zangu zote za filamu na
kunitangaza kimataifa hata show ya London wao ndio wamenitafutia na pia
kuna mambo mengine mengi ambayo yanakuja kwa jinsi walivyoniambia.
Nimeona umuhimu wa kumuenzi Mwl Nyerere kwasababu bado kuna watu na
watoto wanataka kujua Nyerere ni nani na alifanya vitu gani,kama mimi
nitahakikisha kila mwaka ninatoa filamu moja ambayo itakuwa inaelezea
mambo mbalimbali na hotuba zake.”
No comments:
Post a Comment