15 November 2013

PAGE YA FACEBOOK YA ACTRESS SALMA JABU NISHA YAHAKIWA(HACKED) KWA HIYO KUWA MAKINI NA MATAPELI.

Page ya facebook ya muigizaji Salma Jabu Nisha imehakiwa(hacked) na matapeli au watu wanaotaka kumchafua na wameanza kuweka picha chafu na za kimahaba akiwa na Nay Wa Mitego. Nisha
mwenyewe amezungumza na Swahiliworldplanet kwa masikitiko makubwa kwa wanao upload picha hizo hawamtendei haki kwani baadhi ya watu  na mashabiki wake wengine wanadhani ni yeye kweli ila wale wenye upeo na mambo ya mitandao wameanza kuelewa kuwa sio yeye. Page yenyewe ni hii hapa NISHA

Bado tunaendelea kufuatilia na Nisha akifanikiwa kuirudisha page yake kupitia wataalam wa IT basi tutakupa taarifa hapa hapa  ila kwasasa ujue kuwa kinachowekwa katika page ya muigizaji huyo sio yeye.


No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname