15 November 2013

HUZUNI...Huyu ndiye Binti wa miaka 19 asiye kuwa na Uke

article-2507167-19695E1300000578-120_636x427
Na Damas Makangale, Moblog kwa Msaada wa Mtandao
Msichana Jacqui Beck (19) ni mtoto wa kike ambaye amezaliwa bila kiungo muhimu cha Mwanamke (Uke) na hawezi kufanya ngono au kupata Watoto kutokana na kukosekana sehemu yake ya Kike kama walivyo wanawake wote hapa duniani.
Beck amesema kuwa alikwenda kwa madaktari kwa ajili ya uchunguzi na wataalamu
wamegundua baada ya vipimo kwamba msichana huo hana Ovary, hana mfuko wa Uzazi wala Uke na hapati hedhi kila mwezi kama wanavyopata Wanawake wenzake duniani.
Anasema alipata mshtuko baada ya kuambiwa na madaktari kwamba hana Uke wala sehemu ya siri haiwezi kufunguka na hiyo alikuwa na umri wa miaka 17 tu.
article-2507167-1968D51000000578-570_634x665
Beck aliendelea kusema wakati akihojiwa na waandishi wa habari wa gazeti la Daily Mail nchini Uingereza kwamba kwanza alikwenda kwa daktari wake kuhusu maumivu ya nyuma ya mgongo na alikuwa hapati kabisa hedhi lakini akitaka kujisaidia haja ndogo anaweza,” alisisitiza
 Uchunguzi wa madaktari umebaini kuwa hali yake si ya kawaida kwa sababu sehemu ya Uke wake ipo kama giza au hamna kitu lakini haja ndogo inatoka lakini hawezi kabisa kufanya mapenzi au kubeba ujauzito.
Madaktari wanasema kwa Wanawake na kwa hali ya kawaida kabisa itaonekana nje –  lakini kwake ni kama hamna kitu bali ni sehemu tupu, msichana huyo Beck anatoka kisiwa cha Wight yeye mwenyewe anasema anajisikia kama kituko kwenye jamii.
article-2507167-1968D51C00000578-746_306x423
Wataalamu wanasema kwamba si jambo la kawaida kwa mwanamke (Abnormality) kwa mtoto wa kike kuzaliwa hivyo lakini kati ya Wanawake 5000 wanaozaliwa mmoja kupata tatizo hilo nchini Uingereza.
Wanawake wanaosumbuliwa na hali kama hiyo kwa kawaida Ovary hawana lakini kupata dalili ya kubalehe si kupata siku zao za kila mwezi au kupata ujauzito

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname