Mwanamuziki
nyota wa muziki wa kizazi kipya usiku wa kuamkia Jumatatu alionja joto
ya kiwe baada ya kutekwa na kusurubiwa kisha kunyang'anywa kila kitu
pamoja na gari yake.XDEEJAYZ inakupa mchongo mzima.
Mwanamuziki
huyo akiwa kwenye viunga vya Club ya usiku ya Kibo iliyopo Tegeta
Jijini Dar pamoja masisita du wakila bata ghafra kundi la watu watano
lilimvamia na kumkamta msobe msobe hadi nje ya ukumbi pamoja na
kumrukisha kichurachura huku wakina dada waliokuwa wamendamana nao
wakilia kwa uchungu kwa kumuonea huruma.
Habari
zaidi toka kwa chanzo chetu cha Xdeejayz kilichoshuhudia timbwiri hilo
kilisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni kudaiwa kwa Matonya na mtoto wa
mjini aliyefahamika kwa jina la Evance" Huyu Evance ni mtoto wa mjini
na huwa anawakopesha pesa wanamuziki mbalimbali pamoja na wasanii wa
bongo movie hivyo miezi ya hivi karibuni alimkopesha shilingi laki nne
msanii huyo kwa madai kuwa hakuwa na pesa ya kula bata wikiendi ambapo
baada ya kumkopesha msanii alianza kuzungusha kurudisha hali iliyomfanya
Evance kuchukua hatua za kumfanyia unyambilisi huo" Kilisema chanzo
chetu
Hata
hivyo baada ya kumkamata msanii huyo Evance alimpelekwa Oysterbay
ambapo aliiacha gari na simu kwa makubaliano atakapoleta pesa hiyo
atapewa gari yake.
No comments:
Post a Comment