18 November 2013

MTOTO ALIYE KUFA NA KUDAAIWA KUFUFUKA ANENA KWA MARA YA KWANZA...AFUNGUAKA KILICHOMKUTA NA ALIKUWA WAPI BAADA YA KUFARIKA TOKA MWAKA 2011

   
Ni hivi karibuni, Mji wa Geita na maeneo jirani ulikubwa na taharuki ya aina yake,pale mtoto Shabani Maulid (15) anaedaiwa kwamba alifariki dunia miaka miaka mitatu iliyopita, alipoonekana akiwa hai katika Kijiji cha 14 Kambarage, Mtaa wa Mbugani.
 Tukio hilo lilizua hofu kwa wakazi wa Mji wa Geita huku waliowengi wakitaka kujua mtoto huyo aliyekutwa amefariki dunia baada ya kupotea kwa siku nne mwaka 2011 na mwili wake kuzikwa, inakuwaje leo hii anaonekana akiwa hai?
 Tukio hilo lililotokea Septemba mwaka huu linashuhudiwa na wazazi wa Shaban, ndugu zake, jamaa na hata majirani wa eneo hilo ambao pia wanahoji, je aliyezikwa wakati mwili wa mtoto huyo ulipookotwa ni nani na je mwili wake uko kaburini au la?
 Maswali haya na mengine, yalikosa majibu kwani baada ya kuonekana kwake, Shaban hakuweza kuongea vizuri na alionekana kutofahamu kabisa Kiswahili, lugha ambayo kabla ya kutoweka kwake aliifahamu vyema. Wakati huu mtoto huyu anaongea Kiha, japo nayo kwa tabu.INAENDELEA

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname