Bondia
aliyetisha sana enzi zake na kuporomoka ghafla kabla hajachukua uamuzi
wa kustaaf mchezo wa masumbwi Mike ‘Iron’ Tyson ameeleza ukweli kuwa
alikuwa anatumia dawa za kulevya wakati wa mapambano yake yote makubwa.
Tyson
ameanika ukweli huo kwenye kitabu chake ‘Undisputed Truth’ ambapo
amesema alikuwa anatumia uume wa bandia kukwepa vipimo vya kuangalia
kama ametumia madawa ya kulevya ambavyo vilikuwa vinachukuliwa kwa njia
ya kupima haja ndogo.
“I
had to use my whizzer, which was a fake pen*s where you put in
someone’s clean urine to pass your drug test.” Ameandika Tyson.
Mike
Tyson amefunguka jinsi alivyokuwa akiwachezesha wapimaji ambapo siku
zote alikuwa anatumia uume wa bandia uliojazwa haja ndogo ya mtu
mwingine katika timu yake, na kisha kuzuga kama anautoa mwenyewe hivyo
vipimo vinakuwa fake.
Tyson
amesema alikuwa anatumia dawa za kulevya aina ya Cocain na Marijuana
mara kwa mara, na akakumbushia moja kati ya situation alizokuwa amevuta
ni pale alipokuwa ameenda kwenye press conference na Lennox Lewis huko
New York, mwaka 2002 ambapo alitaka kumvaa Lenox pale pale.
“I lost my mind,” Tyson recalled. “I looked over at him and wanted to hit the motherf---er.” Yanasomeka maandishi ya Tyson
No comments:
Post a Comment