25 November 2013

MAIMARTHA, ASHA BARAKA NGOMA NZITO!!!! FUATILIA ZAIDI



KESI ya Mtangazaji Bongo, Maimartha Jesse na Mkurugenzi wa Bendi The African International ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka bado kazi nzito ambapo mshtakiwa (Maimartha) ametakiwa kupeleka ushahidi mahakamani.
Asha Baraka.
Akizungumza kwa masikitiko, Maimartha alisema anaendelea kusubiri siku hiyo ya kupeleka ushahidi ifike kwani anaamini hana makosa kwa sababu hajawahi kumdhalilisha kokote kama alivyoshtakiwa.
“Asha Baraka anataka nimlipe milioni tano sasa sijui hizo fedha zote zimetokana na nini na itakuwaje maana kama ni kudaiana na mimi nitamdai kimwana wangu anayecheza shoo kwake,” alisema Maimartha.
 

Maimartha Jesse.
Kesi hiyo ya madai inaendeshwa katika Mahakama ya Mwanzo, Kinondoni, Asha Baraka amemshtaki Maimartha kwa kile kilichodaiwa kuwa alimdhalilisha kwenye vyombo vya habari, kesi hiyo itatajwa tena Desemba 19, mwaka huu.

-GPL

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname