Mahakama ya mwanzo Kawe jijini dar es
salaam imetoa hati ya kumkamata miss tanzania 2006 Wema Sepetu kutokana
na kile kinachoelezwa kuwa ni dharau ya wito wa mahakama hiyo.
Chanzo cha ndani kilichoomba kuhifadhiwa
ya jina kimempasha mwandishi wetu kuwa hati hiyo ilitolewa mwishoni mwa
wiki iliyopita baada ya wema kushindwa kuhudhuria kesi yake iliyopo
mahakamani hapo na bila kutolewa udhuru wowote.
Aidha imeelezwa kwamba mahakama hiyo pia
imetilia mashaka udhuru uliotolewa septemba 30 kwamba wema ni mgonjwa
baada ya kuvuja kwa picha katika mitandao zikimuonyesha Wema akila bata
Hong Kong China na mpenzi wake wa zamani mwanamuziki Diamond.
Wema alitolewa udhuru huo na kijana aliefahamika kwa jina la Martini .
Kesi inayomkabili wema katika mahakama
hiyo ni ya kumtukana matusi ya nguoni pamoja na kumpiga meneja wa hoteli
ya Mediteranian iliyopo Kawe beach jijini Dar es salaam bwana Godluck
kayumbu.
Baada ya kupata taarifa hizo mwandishi
wetu alimtafuta mlalamikaji wa kesi hiyo bwana Kayumbu na kumuuliza
kuhusu hati iliyotolewa na mahakama ambapo alithibitisha kuwepo kwa
jambo hilo.
Bwana Kayumbu alisema kuwa amepewa hati
maalum ya kumkamata wema octoba 30 mwaka huu ambayo kesi hiyo ilitajwa
tena mahakamani hapo.
Alisema kuwa Wema Sepetu anaweza
kukamatwa muda wowote kuanzia sasa kwani octoba 30 mwaka huu kesi hiyo
ilitajwa tena mahakama ya Kawe chini ya mheshimiwa hakimu Ikanda lakini
wema hakutokea na hakuna mtu yeyote aliyekuja kwaajili ya kumtolea
udhuru.
Kayumbu alibainisha kuwa mshtakiwa wake
wema sepetu hakuja mahakamani mara mbili mfululizo kuanzia septemba 30
2013 na kudaiwa kuwa anaumwa lakini picha zake katika mitandao
zilimuonyesha akitanua hong kong china na mara ya pili kesi hiyo
ilitajwa octoba 30 2013 ambapo hakutokea mtu yeyote anayemuhusu wema
katika mahakama hiyo.
"Kesi ilikuwa ya kwanza kutajwa lakini
nilikuwa peke yangu sasa nikaamuliwa mimi nipewe hati maalum ya
kumkamata wema ambapo nilipewa na nimeshaikabidhi kituo cha polisi cha
kawe kwa utekelezaji maana naona muda unazidi kwenda na kesi haiishi,"
alisema kayumbu.
Mwandishi wetu alipomtaarifu bwana
kayumbu kuwa octoba 30 Wema Sepetu alikuwa kwenye msiba baada ya kufiwa
na baba yake mzazi mzee Isaac Sepetu na kwamba siku hiyo alikuwa
safarini kwenda zanzibar kwa ajili ya mazishi ya mzazi wake huyo, bwana
kayumbu alisemaa kuwa suala hilo halimuhusu kwani hata yeye amefiwa na
wazazi wake.
"Kama kafiwa hata mimi nimefiwa na baba
na mama yangu pia, kinachotakiwa ni kutii sheria za nchi ikiwemo
mahakama ,kama alifiwa kwanini asitoe udhuru? sina mazungumzo tena
kinachotakiwa ni sheria ichukue mkondo wake, popote atakapopatikana wema
ni lazima akamatwe," alisema Godluck.
Wema hakupatikana kwenye simu ili kuzungumzia jambo hilo.
No comments:
Post a Comment