Muigizaji wa filamu nchini Elizabeth Michael aka Lulu amekanusha fununu zilizoandikwa kwenye gazeti la udaku liitwalo ‘Filamu’ kwamba amechumbiwa na muda mchache ataolewa.Akizunguza jana kwennye kipindi cha XXL cha Clouds FM, muigizaji huyo wa Foolish Age, alisema hajachumbiwa na mtu yeyote ila ni magazeti ya udaku tu ndio yamekuwa yakiandika kile yanachojisikia.

“Mimi sijachumbiwa na hakuna mtu yeyote aliyenichumbia na kama
itatokea siku nikachumbiwa kila mtu atajua, na ni mimi mwenyewe ndiye
nitakaesema,” alisema mrembo huyo.
“Lakini sasa sijajua wao wamepata hiyo habari kutoka kwenye chanzo
gani, by the way kwaajili kumekuwa na habari kila kukicha kila mtu
anayejisikia kuandika anaandika ,anaamka anaandika, anaamka anandika.
"Kwa hiyo leo wameandika nimechumbiwa, kesho wataandika nimeolewa, kwa hiyo
inategemea na mood ambayo wao waliamka nayo, kwamba ‘leo Lulu
tumchumbie, tumuozeshe, tumuachishe’, I don’t know.
“Kuchumbiwa, kuolewa,kuwa mke ni vitu ambavyo tumeumbiwa binadamu,
vipo kama ukiwa mpango wa mwenyezi Mungu nitachumbiwa na nitaolewa.” Lulu
No comments:
Post a Comment