17 November 2013

KUTOKANA NA PICHA YAKE YA UTUPU KUSAMBAA MTANDAONI, KOLETHA AFUNGUKA NA KUSEMA HAYA...!!

 
Stori: Chande Abdallah
MWIGIZAJI Koletha Raymond ‘Koletha’ amefunguka kuwa hapendi umaarufu kwa kupiga picha za utupu kama wasichana wengi walio katika tasnia ya filamu wafanyavyo.

Koletha aliyasema hayo ikiwa ni siku chache tu baada ya mitandao kadhaa kusambaza picha ya utupu inayoonesha sehemu ya kiuno, ikidaiwa kuwa ni ya msanii huyo ambapo paparazi wetu alipomhoji kuhusiana na picha hiyo, alitiririka:

Hiyo picha siyo yangu. Mimi siwezi hata siku moja kusaka usupastaa kwa kupiga picha za uchi, kwanza sipendi na sitaki kufanya hivyo sababu ninajiheshimu tofauti na wenzangu wanaoendekeza mambo hayo wakati hawana kazi hata moja sokoni,” alisema Koletha.

1 comment:

  1. Ni vizuri kujiheshimu na kulinda uzuri wako wa asili

    ReplyDelete

Comments system

Disqus Shortname