Msanii aliyejipatia umaarufu sana kwa kuigiza kama tapeli
ndani ya Bongo Dar es Salaam ‘Dude’, ameonesha kutoelewa kile
kinachofanywa na wasanii wa Bongo Movie wa sasa katika kuhakikisha
wanaipeperusha bendera ya Tanzania katika anga za kimataifa.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, Dude ameeleza kuwa marehemu Steven
Kanumba ndiye muigizaji pekee wa Bongo ambae aliitumia vyema fursa yake
katika kuitangaza Tanzania kimataifa.
“Mimi nadhani ni msanii mmoja, hayati Steve Charles Kanumba ambaye
alikuwa akitumia fursa yake vizuri kujitangaza na kutangaza soko la
filamu hapa nchini. Lakini kwa sasa hakuna kitu chochote kinachoendelea
kwa wasanii wengine na ndio maana unakuta soko letu haliwezi kujulikana
kimataifa.” Alisema Yahaya Dude.
Kwa upande mwingine, Dude alitoa mtazamo wake kuhusu ujumuishwaji wa wasanii wachanga katika tasnia ya filamu nchini.
“Unajua tasnia ya filamu inazidi kukua ila bado kuzalisha wasanii
wachanga wazuri (Upcoming Artist) ukiachana na wasanii wakongwe kama,JB,
Vicent Kigosi (Ray), Wema Sepetu, Rich toka tuwaona enzi hizo kwenye
tamthilia ya ‘Mambo Hayo’ lakini kwa sasa hakuna wasanii wazuri wachanga
.”
Lakini pamoja na kuona hakuna muamko kwa wasanii wachanga, Dude
anaona hali ni mbaya zaidi kwa wasanii wa kiume wanaochipukia kwa
kulinganisha na waanii wa kike.
“Afadhali hawa kidogo wakina Irene Uwoya,Rose Ndauka,Jackcline
Wolper, kwa upande wa wanaume sijaona bado kama kuna wasanii wachanga
wanaoweza kutufanya sisi wakongwe tuwe na hamu ya kusema kweli filamu
yetu ina vipaji vipya na wasanii wakali.” Alisema Dude.
Source: Times Fm
No comments:
Post a Comment