Mwamba wa Kaskazini Joh Makini ambaye aliungana na wasanii
wa kundi la Weusi Jumamosi (November 23) na kudondosha show kali na
kulipamba tamasha la ‘P-Square Live In Dar’, ameeleza vitu alivyojifunza
kwenye performance ya wasanii hao ndugu toka Naija, Peter na Paul.
Joh ameiambia tovuti ya Times fm kuwa amejifunza zaidi jinsi ya
kuwasiliana na audience wake wakati anaimba jukwaani na kuwafanya wawe
wajisikie kuwa sehemu ya show.
“Kitu ambacho nimejifunza ni kwamba kuendelea kuongeza confidence na
jinsi ya ku-communicate na fans unapokuwa jukwaani ndio kitu kikubwa
zaidi kwenye show mbali na muziki unaokuwa unaufanya pale. Kuongea na
watu na kuwacheck wako kwenye mood gani na kurelax kwenye stage ndio
kitu ambacho nimejifunza. Kwa sababu hata ukiangalia show ya P-Square
utagundua wao wana confidence wanapokuwa kwenye jukwaa wanaongea na
watu. Inawafanya fans wanajisikia wako na wewe kwenye lile tukio sio tu
unapiga wimbo baada ya wimbo unaondoka.” Ameeleza kaka yake Nikki wa
Pili.
Akasisitiza, “Kwa hiyo communication kati ya msanii na mashabiki ni
kitu muhimu sana na ndio kitu ambacho ninaendelea kujifunza kila siku
kwenye show zangu.”
Tovuti ya Times fm ilitaka kufahamu maoni ya Joh Makini kwa upande
wake kwa jinsi alivyoiona show hiyo kwa kulinganisha na show nyingine
zilizowahi kufanyika Tanzania, kama hiyo anaweza kuiita ‘show bora
zaidi’ kati zote alizowahi kuona za kimataifa hapa Tanzania.
“Kiujumla tamasha lilikuwa kubwa, na ni one of the biggest shows
ambazo nimeziweka kwenye historia yangu. Performance yao ilikuwa nzuri
lakini naamini kwamba tunaweza kufanya bigger than that kama
tukiwezeshwa vizuri financially.” Amefunguka Joh Makini.
Joh amedai kuwa show hiyo haikumshangaza kwa kuwa anaamini kuwa
walistahili kufanya vizuri hata zaidi ya walivyofanya kutokana na
treatment wanazozipata kama wasanii wa kimataifa.
“Kwa hiyo sijashangaa, yaani hawajafanya kitu cha kunishangaza kwa
kuwa naamini kwamba wanalipwa vizuri. kwa hiyo walistahili kufanya kile
kitu walichokifanya kutokana na jinsi ambavyo wanapewa treatment kama
wasanii wa kimataifa. Na nilitarajia labda watafanya hata zaidi ya kile
ambacho nilikiona kutokana na treatment ambayo wanapewa kama
International artists.
“Kwa hiyo nilichokiona pale ni kwamba tunaweza kufanya vizuri zaidi
ya tulivyofanya, ama hata zaidi ya wasanii wengi wa kimataifa kama
tutawezeshwa.” Ameeleza Joh Makini.
P’ Square walipewa kampani ya kutosha na wasanii wa hapa nyumbani
Tanzania, Lady Jay Dee, Ben Pol, Joh Makini akiwa na kundi la Weusi na
Profesa Jay.
No comments:
Post a Comment