Tume ya
Mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania imepata pigo baada ya mmoja wa
wajumbe wake Dr. Sengondo Mvungi kufariki dunia nchini Afrika Kusini,
ambako alikuwa akitibiwa.Dr.
Mvungi, alipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi baada ya kuvamiwa
na watu wanaoaminika kuwa majambazi nyumbani kwake mjini Dar, es Salaam,
wiki iliyopita.Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
Bw. Assaa Rashid Dkt. Mvungi alifariki majira ya saa 8:30 mchana kwa
saa za Afrika ya Kusini akiwa katika Hospitali ya Milpark.
"Kwa
masikitiko makubwa, Tume inawafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake, Dkt.
Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Hospital ya Milpark
iliyopo jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini amefariki dunia leo
Jumanne, Novemba 12, 2013 saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini,"
amesema Bwana Rashid katika taarifa yake fupi.
Amesema taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Afrika Kusini kuja nchini Tanzania kwa mazishi zinaendelea.
Marehemu
Dkt. Mvungi alisafirishwa siku ya Alhamisi, Novemba 7, 2013 kwenda
nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo
cha Mifupa Muhimbili (MOI) alipokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani
kwake.
Dkt.
Mvungi pamoja na kuwa ni mwanasheria aliyebobea katika fani ya Katiba,
pia ni mwanasiasa ambaye aliwahi kugombea urais mwaka 2005 kupitia chama
cha NCCR Mageuzi.
No comments:
Post a Comment