13 November 2013

CHAZ BABA APATA AJALI YA PIKIPIKI....

Chaz Baba akiuguza majeraha aliyoyapata
Risasi Vibes lilifunga safari hadi nyumbani kwake Mwananyamala, Dar kumjulia hali ambapo alisema tukio hilo lilitokea katikati ya wiki iliyopita, Ubungo baada ya kugongwa na gari kwa nyuma.
“Nilikuwa natokea Kimara, nikiendesha pikipiki yangu. Si unajua tena ile barabara ipo kwenye matengenezo kwa hiyo
vizuizi ni vingi njiani. Ghafla nilishangaa pikipiki ikigongwa kwa nyuma, nikaanguka.

“Namshukuru Mungu maana mazingira niliyopata ajali ni mabaya sana isitoshe unajua pindi upatapo ajali kuna wengine wanakuja
kukusaidia na wengine ni wezi lakini sikuibiwa kitu.

“Nimeumia mkono, kiuno, mguu mmoja wa kushoto na maumivu kwa ndani lakini hakuna sehemu niliyovunjika,” alisema Chaz Baba

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname