Mtoto Omar Said
Katika hali Isiyo ya kawaida, wala kufikirika Baba mmoja aliyekuwa
akiishi na binti mmoja jina Hamida, na mtoto wake mmoja Omar Said ,
alijikuta akichukua kiberiti na mafuta na kumchoma Binti huyo kama
karatasi. Kisa kizima hichi hapa mtoto akisimulia:
"Tulikuwa tumelala usiku mimi na mama tu chumbani, kwani ilikuwa ni
kawaida baba kuchelewa kurudi na mara nyingi huwa anarudi akiwa amelewa
na kumpiga mama kila siku , mama anapiga kelele usiku mpaka baba mdogo
anayeishi jirani huja na kuingilia ugomvi" Mtoto akiendelea kusimulia akiwa anabubujikwa na machozi:
"Siku hiyo baba alirudi usiku sana akiwa amelewa kama kawaida yake
akamuamsha mama, halafu nikamsikia anamuambia mama kwenu siendi na kama
utaendelea kunilazimisha nitoe mahali basi leo ndio mwisho wako,
nikasikia tu mama amepiga kelele kubwa ambayo sio ya kawaida, mara
nikaona kama moto mkubwa ndani nikaamka na mimi nikaanza kupiga kelele
nilipo angalia vizuri nikaona kumbe ni mama yangu anateketea na moto
niliendelea kupiga kelele lakini mama yangu wakati huo alikuwa
ameshanyamaza haoengei tena, siku hiyo sijamuona hata baba mdogo kuja
kuamualia, baba alikimbia sikumuona tena hadi leo"
No comments:
Post a Comment