BAADA YA HABARI KUENEA KWAMBA HUYU DADA NDO KAVUNJA NDOA YA BOB JUNIOR...HATIMAYE UKWELI WAJULIKANA
 |
| Bob Junior na Ashley
|
Mwanamuziki maarufu wa Bongofleva Bob Junior amekana habari zilizoanza
kusambaa mitandaoni kuwa yupo kwenye dimbwi la mapenzi na Ashley Toto
ambaye ni muigizaji wa filamu za Kiswahili kutoka Kenya lakini akiwa na
makazi yake nchini Ujerumani, Ashley pia ni promota wa muziki na amekuwa
akifanya kazi na wasanii mbalimbali wa Afrika mashariki kwa kuwapeleka
ujerumani kufanya shows na kwasasa yupo Kenya. Habari ni kuwa hata ndoa
ya Bob Junior imevunjika kisa kikiwa ni wawili hao kujinafasi kwa raha
zao. Baada ya habari hizo kuanza kuenea na kufika hapa Swahiliworldplanet
ilibidi kuwatafuta wasanii hao wawili ili kuwauliza kuhusu issue hiyo
na wa kwanza kupatikana alikuwa ni Ashley ambaye alitumiwa ujumbe juzi
kuhusu kuwa mapenzini na Bob Junior na alijibu kwa ufupi "sijui lolote
samahani" na alipobanwa zaidi alisema "sisi sio wapenzi we are just
friends ....more information muulize mwenyewe"
Baada ya hapo ilibidi kumgeukia Bob Junior na kumtumia ujumbe jana ila leo akajibu ujumbe huo kwa kusema "hapana
si kweli, hata blog iliyotoa habari hiyo inaitwa Udaku blog so nadhani
ushajua hakuna ukweli". ilipomuuliza kwa hiyo upo na mkeo Halima(ambaye
ni muigizaji wa filamu) kama zamani hamna tatizo lolote alijibu kwa
kusema "kwa sasa sina mke kaka nipo single"
No comments:
Post a Comment