Dar es Salaam Octoba 4, 2013:Azam
Media Limited imefanikiwa kukamilisha utaratibu wa ushirikiano na
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) utakaowawezesha mashabiki wa
kandanda kote nchini kunufaika kwa kuona michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom
kila mwishoni mwa juma hadi kukamilika kwa nusu ya msimu wa 2013/14
kupitia TBC1 kwa hisani ya AzamTV.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi (Kamati ya Ligi) wameeleza kuunga mkono utaratibu huu makini.
“Baada ya kupata haki za matangazo ya luninga ya Ligi Kuu ya Vodacom, moja ya shabaha zetu kuu imekuwa ni kuhakikisha kuwa tunafanikiwa kurusha matangazo yanayokidhi viwango vya kimataifa kwa ubora. Ili kufanikisha shabaha hiyo tumewekeza vilivyo katika teknolojia ya kisasa ya vifaa vya matangazo ya nje (Outside Broadcasting) na katika mafunzo kwa watumiaji wa vifaa hivyo. Ninayo furaha kusema kuwa matayarisho yamekwenda vema kiasi kwamba tumejikuta tuko tayari kurusha matangazo ya kiwango cha juu kabla hata ya kuzinduliwa kwa huduma kamili za AzamTV”, alisema Rhys Torrington, Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited.
Mara tu huduma kamili za AzamTV zitakapozinduliwa majuma machache yajayo, matangazo ya michezo ya Ligi Kuu kwa wigo mpana yatakuwepo pia kwenye chaneli yake hadi mapumziko ya nusu msimu. Baada ya hapo matangazo ya Ligi Kuu ya Vodacom yatapatikana kwa wale tu watakaokuwa na visimbuzi (decorders) vya AzamTV
No comments:
Post a Comment