25 October 2013

KING MAJUTO ALIPWA MILIONI 17 MPAKA 20 KWA MWEZI KATIKA FILAMU

King Majuto
King Majuto ambaye ni muigizaji wa filamu wa siku nyingi nchini na mmoja wa mastaa ambao filamu zao zinauza vizuri sokoni ameelezea kipato chake anachokipata kwa mwezi kutokana na uchezaji wa filamu. Akizungumzana na Millardayo King Majuto alisema "kwenye movie za kuigiza sasa hivi kama mtu akitaka kunishirikisha ni lazima unilipe milioni nane kutoka milioni 2 au tatu nilizokua nazikusanya mwanzoni, hii bei nimeibadili kuanzia mwezi September 2013, mimi kadri ninavyocheza movie nyingie za kushirikishwa ndio nazidi kujipunguzia kipato changu kwa mwezi kutoka kampuni ya STEPS iliyoniajiri"

Muigizaji huyo wa siku nyingi aliyehamasisha wasanii wengi wa sasa kujitumbukiza kwenye sanaa aliendelea kwa kusema "Mpaka sasa nimecheza movie zaidi ya 600 toka nimeanza kuigiza za kushirikishwa na zangu mwenyewe, nilianza kulipwa zaidi ya milioni moja kwenye movie toka mwaka 2007/2008 baada ya kuwa na kampuni ya Ally Riyami ambae alikua ananilipa shilingi laki sita kwa kila movie ya Comedy kwa hiyo kwa mwezi napata mpaka kwenye milioni 6 au saba kutokana na idadi ya movie nitakazoigiza"
Majuto ambaye anawatoa jasho mastaa vijana sokoni alimalizia kwa kusema " kwa sasa hapa Steps nalipwa kuanzia milioni 17 mpaka 20 kwa mwezi, ni malipo mazuri sana ambayo napata kila mwezi na nimepangiwa kucheza movie 9 kwa mwaka lakini kule Ally Riyami kwa mwezi ndio nilikua nacheza hizo movie 10, yaani unacheza movie nyingi mpaka unasikia kizunguzungu…. kwa sababu nilitakiwa kucheza movie 1 kila baada ya siku tatu ila kwa sasa kwenye mkataba wa Steps nacheza movie moja ya kampuni na moja ya nje ya kampuni, maisha mazuri"

Si kipato kidogo kwa tasnia yetu kwasasa ingawa unastahili zaidi ya kipato hicho kwa mwezi ila ni matumaini yetu malipo yataongezeka tu kwa kadri siku zinavyokwenda na tasnia kuzidi kukua.
                                                 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname