25 October 2013

DINI YA AJABU YAANZISHWA HUKO MBEYA

Diniinayoamini katika MUNGU lakini ikiruhusu yale ambayo dini zingine 

zinapinga imeanzishwa eneo la mji mdogo wa Makongolosi wilayani Chunya 
mkoani Mbeya,
Dinihiyo haiamini katika kutoa sadaka bali inasema tunamtolea nani sadaka 
wakati Vitu vyote tulivyonavyo ni mali ya MUNGU,kwa nini tunampa MUNGU 

mali zake Mwnyewe.!
Dinihiyo inaruhusu ulevi,uchawi na uzinzi kwa sababu vimeumbwa na 

MUNGU,Vile vile inaamini hakuna dhambi duniani,Dini hiyo inaitwa DIMAYO,
sasa imeanza kuenezwa Mbeya

=========================
Ufafanuzi
=========================
By GAMBISHI DWESE
Yawezekana
kweli Bwana Domy umekutana nami. Mimi Ndiyo PAPA-DIMAYO 1: GAMBISHI 
DWESE,( nabii wa kwanza wa DIMAYO) hata hivyo pengine umeninukuu 
kimakosa.Kwanza kabisa Dimayo haiamini katika uwepo wa mungu muumbaji 
aliye hai wala aliyekufa anayedaiwa kuhusika na kila kinachoendelea 
ulimwenguni.
Na
nimeshatoa kitabu kinachoitwa HAKIKA HAKUNA MUNGU MUUMBAJI ALIYE HAI 
WALA ALIYEKUFA anayehusika na kila kinachoendelea. kijitabu hiki 
kinaeleza kinagaubaga kwanini Dimayo haiamini katika uwepo wa mungu 
muuumbaji. nikipata nafasi nitakiingiza kwenye mtandao ili watu wengi 
wakisome.
Ni
kweli hakuna kitu Dhambi bali kuna makosa. na kosa linaweza kuwa kosa 
kulingana na mazingira na wakati katika jamii tofauti. Na ni kweli 
kwamba dini yetu ni ya starehe wala si ya mateso, maana tunaamini hakuna
maisha zaidi ya haya tuliyonayo. Dimayo haijampa mtu ruksa ya kuvunja 
kanuni halisi asili wala sheria halali ya serikali yake halali na wala 
haina upotoshaji hata kidogo. 
Kinachoitwa
sadaka kwetu huwapa watu wenye matatizo. Ni kweli kuna michango mingine
lakini ni ya hiari na ni kwa ajili ya ushirika. Ni kweli kwenye JUMADI 
(jumba la makutano la Dimayo kutakuwa na kaunta ya vinywaji). unajua 
kunywa na ulevi ni vitu viwili tofauti; ulevi ni tabia ya mtu ya kutumia
vileo kupindukia, lakini kwetu tunasema kunywa uwezavyo ilimradi huumii
wala kuumiza vyote kisaikolojia na kimwili, kwa mantiki hiyo ulevi 
kwetu noma ila unywaji ni safi.
Uchawi
ni sayansi, ila utumike kwa faida siyo kwa kuleta madhara. kuwaambia 
watu eti acheni ngono eti mungu hapendi wataacha?. wambie wafanyeje 
ngono kulingana na wakati na mazingira. Dimayo inamfundisha mtu kutenda 
inavyofaa yanayofaa kutendwa kwa kufuata kha na kahaka.


Anyway nashukuru kwa kuianzisha mada hii, nafikiri nitachukua nafasi kuielezea zaidi kila inavyowezekana.


Nina uhakika kwa mtu yeyote mwenye uwezo mkubwa wa kutumia akili zake hawezi kupingana hata kidogo na DIMAYO.


-JF

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname