Marejeo hayo
yanatarajiwa kusikilizwa na Jopo la Majaji watatu wa mahakama hiyo ambao
ni Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati. Katika hukumu
hiyo iliyotolewa Februari 2010,mahakama hiyo iliridhia hukumu ya kifungo
cha maisha kwa Babu Seya na mwanawe, Papii Nguza huku ikimuwaachia huru
watoto wawili wa Babu Seya, Nguza Mbangu, na Francis Nguza.
Juni 25, 2004
Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kusutu, Dar es
Salaam,iliwatia hatiani Babu Seya na wanawe Papii Nguza ‘Papii Kocha’,
Nguza Mbangu na Francis Nguza kwa kupatikana na hatia ya kubaka na
kulawiti.
Januari 27
mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo
alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu iliyotolewa na
aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Addy
Lyamuya ambaye aliwatia hatiani kwa makosa yote waliyokuwa wameshitakiwa
nayo Juni 25 mwaka 2004.
Babu Seya na
wanawe walidaiwa kutenda makosa 10 ya kubaka watoto wenye umri kati ya
miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike
wenye umri huo huo kati ya April na Oktoba 2003 katika maeneo ya Sinza
kwa Remmy, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment