15 October 2013

HII NDO BARUA ILIYOANDIKWA MIAKA 32 ILIYOPITA MPAKA LEO IPO SAFI NA INASOMEKA..!!

Tarehe 9 ilikuwa ni siku ya barua duniani na kama kawaida yangu ya kupenda kumshirikisha msikilizaji wangu nilipata barua.Barua hii iliandikwa tarehe 29 mwezi wa 10 mwaka 1981 ina maana mwezi huu inatimiza miaka 32.
Barua hii aliandikiwa Charles Chopa akiwa shuleni Lindi.Wakati huo alikuwa na miaka 17 akisoma kidato cha kwanza.Alipotoka nyumbani Dar maeneo ya kariakoo lakini nyumbani aliacha mama mgonjwa.
 Alipopata barua hii akajua sasa mama ndio basi tena.Barua ilifika bado wiki moja kufunga shule.Siku zikaenda hatimae akafunga shule na kurudi nyumbani.Kufika nyumbani mama alikuwa mahututi amelazwa muhimbili na kauli imeshakata kesho yake akafariki dunia.
Ilimuachia simanzi na toka wakati huo hii barua imekuwa sehemu ya maisha yake akipata changamoto za maisha anaisoma imliwaze maana ndio maneno ya mwisho mama yake alimwambia.
Nimejaribu kugeuza picha zikae sawa zimenigomea.Kusoma inabidi usome kiupande upande daah.
Nilifurahi kwa Mr.Chopa kuja kushiriki nasi na kushare barua yake hii ambayo anasema mkewe,watoto wake watatu wanaijua na atatitunza mpaka Mungu atakapomchukua na atawasihi watoto wake waitunze pia.
Je wewe una barua uliyoitunza kwa muda mrefu zaidi ya hapa?kwa nini?

SOURCE: DINA MARIOS

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname